SWALI LA JUMAPILI NA MIMI MWANAKIJIJI
Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?
Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?
Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...