Miongoni mwa Wabunge Viti Maalum ambao hawakupata kuchaguliwa tena ni
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga, Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana na
viongozi wa mikoa wa UWT, wakuu wa wilaya na wabunge kadhaa wa Viti
Maalumu wanaomaliza muda wao.
Mkoani Njombe katika kura za
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana, alijikuta akipoteza fursa ya kurejea
bungeni kupitia uwakilishi wa wanawake wa mkoa huo. Mshindi katika kura
hizo ni Dk Suzan Kolimba, ambaye alijizolea kura 252 na kufuatiwa na
Neema Mgaya 213.
Wengine na kura zao katika mabano ni Dk Chana
(164), Erika Sanga (107), Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sitaki (38)
na Magret Kyando (5).
Katika Mkoa wa Iringa, aliyekuwa Mbunge wa
Viti Maalumu na mmoja wa wenyeviti wa Bunge la 10 linalomaliza muda
wake, Lediana Mng’ong’o (58) naye amepoteza fursa ya kurejea bungeni
kupitia dirisha hilo la UWT.
Aliyeongoza katika kura hizo na
kujihakikishia kuingia katika bunge lijalo ni Rose Tweve, aliyezoa kura
240 na kufuatiwa na Mbunge anayemaliza awamu yake ya kwanza ya ubunge
huo wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati aliyepata kura 199.
Mng’ong’o alijikuta akichukua nafasi ya tatu kwa kupata kura 162 na
kufuatiwa na Shakira Kiwanga (89), Esta Chaula (21), Emma Mwalusamba
(14), Hafsa Mtasiwa (10), Farida Ninje (4) na Agnes Nyakunga (4).
Katika mkoa wa Tabora, ndiko ambako wabunge waliomaliza muda wao,
wamefanikiwa kutetea nafasi yao ya kurejea bungeni. Uchaguzi uliofanyika
mkoani hapo, umeshuhudia Mbunge aliyemaliza muda wake, Munde Tambwe,
akitetea kiti chake kwa kupata ushindi wa kwanza baada ya kuzoa kura
662. Tambwe alifuatiwa na mbunge mwenzake aliyemaliza muda wake, Mwanne
Mchemba, aliyejizolea kura 342.
Wengine walioshiriki katika
uchaguzi huo na kura walizopata ni Aziza Ally (290), Paskazia Malunde
(52), HamidaThabit (40), Asma Suleiyum (40), Nasalile Mwaipase (16) na
Agnes Mgongo (6).
Mkoani Arusha nako, Mbunge wa Viti Maalumu
anayemaliza muda wake Catherine Magige, amefanikiwa kushinda baada ya
kujizolea kura 409, huku mshindi wa pili akiwa Vaileth Mfuko, ambaye
alipata kura 248.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Alphonce
Kinamhala, alitaja wengine katika kundi hilo kuwa ni Flora Zelote (128),
Halima Mamuya (92), Tina Timani (91), Clementina Mollel (44), Rehema
Mroso (9), Nembris Kimbele (44), Catherine Sakaya (6) na Mary Morindet
(51). Katika kundi la wabunge wa Viti Maalumu, aliyeshinda ni Amina
Mollel aliyepata kura 362 na kumbwaga mwenzake katika kundi la walemavu,
Christina Manyenye aliyepata kura (196).
Katika Mkoa wa Mtwara,
aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Anastansia Wambura aliongoza kwa
kupata kura 438 na kufuatiwa na Mbunge mwingine wa Viti Maalumu
anayemaliza muda wake, Agness Hokororo aliyepata kura 316. Hokororo pia
ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma. Msimamizi Mkuu wa uchaguzi
huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT
Taifa, Halima Dendego, alitaja wengine walioshiriki katika uchaguzi huo
na kura zao katika mabano kuwa ni Rukia Swalehe (223), Daisy Ibrahimu
(204), Emma Rashid Kawawa (40), Luckiness Amlima (12), Dk Divana Kaombe
(11),Asha Motto (8) na Thecla Mbuki (1).
Mkoani Singida, mbunge
wa Viti Maalum anayemaliza muda wake, Diana Chilolo, alijikuta
akishindwa kutetea nafasi yake baada ya kuibuka mshindi wa tatu. Mbali
na Chilolo, pia msanii maarufu wa filamu, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka
2006, Wema Sepetu, ambaye alivuma wakati alipochukua fomu, naye
alijikuta akishindwa katika kura hizo. Akitangaza matokeo ya uchaguzi
huo, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko
Kone, alimtaja mshindi wa kwanza kuwa ni Aysha-Rose Matembe aliyezoa
kura 311, huku Mbunge wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake, Martha
Mlata, akitetea nafasi hiyo baada ya kuibuka wa pili kwa kupata kura
235.
Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo na kura zao katika
mabano ni Chilolo (182), Sepetu (90), Sarah Mwambu (74), Martha Gwau
(44), Rehema Madusa (24), Aziza Ntandu (5), Mary Marco (3), Sofia Joseph
(2), Salome Mpondo (1), Leah Samike (1) na Elizabeth Lucas (0). Bukoba
Mkoani Kagera, Mbunge wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake, ambaye pia
amekuwa Mbunge kwa miaka 25, Elizabeth Batenga ameshindwa kutetea nafasi
yake.
Mbali na Batenga, pia Mbunge wa zamani wa Jimbo la Muleba
Kaskazini, Ruth Msafiri, aliyekuwa akiwania kurejea bungeni kwa kupitia
Viti Maalumu, naye ameanguka katika uchaguzi huo. Akitangaza matokeo ya
uchaguzi huo jana, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, John Mongella, alimtaja aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum
mkoa huo kwa miaka mitano iliyopita, Benadetha Mshashu kuwa ndiye
mshindi wa kwanza, baada ya kupata kura 432.
Mshindi wa pili ni
Oliva Semguruka kutoka wilayani Ngara aliyepata kura 314. Wengine
walioshiriki katika uchaguzi huo mbali na Batenga aliyepata kura 255 na
Msafiri aliyeambulia kura 20 ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Janath
Kayandaali (133) na Mwagen Balaganwa (47). Pia yumo Elizabeth Ngaiza
aliyepata kura 16, Levina Jovin ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo
(16), Grace Maumbuka (7) na Domina Balyagati (7).
Morogoro
Mkoani Morogoro wabunge watatu wa Viti Maalumu waliomaliza kipindi chao,
Sara Msafiri, Dk Christine Ishengoma na Margaret Mkanga (Kundi la
Wenyeulemavu), wametetea nafasi zao baada ya kushinda katika kura hizo.
Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajab
Rutengwe, aliwataja Dk Chritine Ishengoma kuwa mshindi kwa kwanza kwa
kupata kura 641.
Aliyeshika nafasi ya pili ni aliyekuwa Mbunge
wa Viti Maalumu kupitia UVCCM Mkoa wa Morogoro, Sara Msafiri ambaye
alichaguliwa kwa kura 608. Wagombea wengine katika kundi hilo ni Harriet
Mwakifulefule, Elizabeth Lyimo, Dk Magdalena Kongera, Sarah Kalaite,
Tatu Madikah, Susan Saileni, Mariam Kiamani, Mercy Minja, Redempta Mushi
na Lucy Ngugi.
Katika kinyang’anyiro cha ubunge viti maalumu
kwa watu wenye ulemavu mchuano, ulikuwa mkali kati ya Mbunge anayemaliza
muda wake, Margaret Mkanga ambaye alipata kuwa 424 sawa na asilimia
55.99 ya kura zote 759 zilizopigwa. Mshindani wake mkubwa muigizaji wa
filamu nchini, Wastara Issa alipata kura 252 sawa na asilimia 33 ya kura
zote huku Chausiku Lukinga akiambulia kura 43.
Mkoani Dodoma,
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalli, Shamsa Mwangunga, alijikuta
akishindwa kufurukuta katika uchaguzi huo, ambao Mbunge wa Viti Maalum
anayemaliza muda wake, Felister Bura, aliibuka kidedea baada ya kupata
kura 457. Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa (UWT) Mkoa wa Dodoma,
Kaundime Kasesa, alimtaja mshindi wa pili ambaye naye ana fursa ya kuwa
Mbunge wa Viti Maalumu, kuwa ni Fatma Tawfiq, ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Manyoni aliyepata kura 368.
Wengine walioshiriki mbali na
Mwangunga aliyepata kura 27 ni Asia Abdalah (112), Fortunata Njalala
(102) na Neema Majure (78). Pia yumo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma,
Salome Kiwaya, Elizabeth Chagwanda, Romana Nyoni na Rahel Baragele.
Wengine ni Mary Chihoma, Sarah Chwamba, Martha Dismas, Aurelia Mamboleo,
Nyemo Masimba, Egla Mwamoto, Judith Muyeya, Mary Mgongo, Safina Mfaki,
Mariam Ndahani, Asha Omary na Stella Mwimba.
Katika mikoa
mingine matokeo ya awali tuliyopata ni Mkoa wa Rukwa ambao aliongoza
Silafi Maufi na kufuatiwa na Bupe Mazengo;Katavi ni Taska Mbogo na Ana
Lupembe; Kigoma ni Josephine Genzabuke na Philipa Mtulano; Kilimanjaro
ni Shary Raymond na Betty Machangu na Tanga ni Naibu Waziri wa Sheria na
Katiba, Ummy Mwalimu akifuatiwa na Sharifa Abebe.
Mkoani Mbeya
mshindi ni Mary Mwanjelwa na Mary Mbwilo; Kaskazini Unguja ni Angelina
Malembeka na Mwanajuma Kassim; Kusini Unguja ni Asha Msimba Jecha na
Mwamtum Haji Dau; Mkoa wa Mjini ni Fakharia Khamis Shomari na Asha
Abdallah Juma na Mkoa wa Mgharibi ni Tauhida Nyimbo na Kaukeb Ally
Hassan.
Katika Mkoa wa Songwe, mshindi ni Juliana Shonza na
Neema Mwandabila; Simiyu ni Ester Midimu na Lea Komanya; Manyara ni
Martha Umbulla na Esther Mahawa huku mkoani Mara washindi ni Agnes
Mathew na Christina Samo. Mkoani Ruvuma, mshindi ni Jackline Mshongozi
na Sikudhani Chikambo; Kaskazini Pemba ni Maida Hamed Abdallah na Asia
Sharif Omary.
Katika Mkoa wa Kusini Pemba ni Faida Mohamed na
Asha Moahamed Omary huku Lindi akipita Hamida Mohamed Abdallah na
Honoratha Chitanda. Katika Mkoa wa Geita, mshindi ni Vicky Kamata na
Josephine Chagulla; Mwanza Kemilembe Lwota na Kiteto Koshuma; Pwani
akipita Zaynab Vullu na Subira Mgalu huku Shinyanga akipita Lucy Mayenga
na Azza Hilary.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment