Bukobawadau

“SIASA ZA BUKOBA” KIGANJANI KWAKO

“SIASA ZA BUKOBA” KIGANJANI KWAKO! Bukoba Wadau Media inapenda kuwafahamisha Wazawa wa Bukoba walioko nje ya Majimbo ya Bukoba kuwa imefungua Jukwaa la Whatsapp kwa jina “SIASA ZA BUKOBA” ili kuwawezesha kupata taarifa za papo kwa papo viganjani mwao juu ya mambo yanayoendelea katika siasa za Uchaguzi Mkuu huku nyumbani.

 Fursa hii inatoa kipaumbele kwa wale walioko nje ya nchi. Kuunganishwa kwenye Jukwaa hili tuma ujumbe wa whatsapp kwenda namba +255 784 505045/+255-684-623-070. Masharti ya kushiriki katika Jukwaa hili ni kama ifuatavyo:

• Kujadili au kushirikishana habari zile tu zinazohusu siasa na mambo yanayoathiriwa na siasa za Bukoba

• Kujadili mada, kupinga au kukubali hoja ziletwazo Jukwaani kwa heshima na staha

• Kutojihusisha kwa namna yoyote ile na uletaji wa mada au kuingiza hoja za kuwagawa wanajukwaa kwa namna yoyote ile; iwe ya kidini, kitabaka au kikabila

• Kutotoa kashfa au kusambaza tuhuma zisizo na ushahidi kwa chama au mgombea wa chama chochote kinachoshiriki Uchaguzi wa Mkuu

• Mwanajukwaa kuwa tayari kuwezesha ukusanyaji wa Taarifa Maalumu itakapohitajika

• Sheria za Jukwaa zinaweza kubadilika au kuongezwa muda wowote kulingana na matakwa ya Washiriki baada ya kuafikiana. Kulingana na wigo mfinyu, tutakuwa na nafasi chache sana za upendeleo kwa Wazawa waliko ndani ya Tanzania. Imetolewa na Bukoba Wadau Media 

Mawasiliano: 0784 505 045 au 0768 397 241
                       0754 505 043
Next Post Previous Post
Bukobawadau