Bukobawadau

SIO RAHISI WOTE TUONE JAMBO KWA WAKATI MMOJA

SIO RAHISI WOTE TUONE JAMBO KWA WAKATI MMOJA
Katika utendaji wa jambo lolote la kijumuia ambamo kuna timu ya viongozi ambao ndio hufikiwa na taarifa zote muhimu na kuelewa uelekeo halisi...sio rahisi watu wote kuona kile walichokiona viongozi.
Kwa kiwango cha taarifa wanachokuwa nacho kulinganisha na washiriki wengine. Itakuwa ajabu kwelikweli kama kila kilichoonwa na viongozi na mwanachama wa jumuia naye lazima awe amekiona.
Hizo porojo hapo juu hazina ishu sana.. Ishu ni kwamba Kwa MwanaCHADEMA/UKAWA ambaye hajaona busara iliyotumika kumpokea Lowassa, hapaswi kulaumiwa sasa. Muda ndio utakuwa mwamuzi mzuri! Huenda kama anakichwa cha kuelewa akajakuelewa baadae safana safari ikiwa inaendelea!!
Unaweza jifikirisha na option sahihi kati ya hizi tatu
1. Lowassa angebakia CCM na kuunganisha nguvu zake kambi ya Magufuli, kwa umoja wao wapambane na UKAWA
2. Lowassa angeenda ACT Tanzania (au Wazalendo ya ZZK) akaongeza nguvu huko na timu yake na wanomuunga mkono ili UKAWA wapambane kwa pamoja na CCM na ACT
3. Lowassa kukaribishwa UKAWA/CHADEMA na kuhamishia nguvu zake na wafuasi wake upande huu ili kukabiliana na CCM na vibaraka wake huku ACT wakikosa hiyo "busti" ambayo waliitegemea kuwazodoa CHADEMA!!
Siku njema
CREDIT TAUSI
Next Post Previous Post
Bukobawadau