Bukobawadau

ZIARA YA FR.JAMES RUGEMALIRA NA WADAU WA VIP KUKAGUA ENEO LA MRADI MKUBWA WA HOSPITAL YA TIBA YA SARATANI MJINI BUKOBA

Mshauri wa kimataifa wa kujitegemea (International Independent Consultant) Fr. James Rugemalira, wa VIP Engineering and Marketing Limited katika picha ya pamoja na washauri wa kitaifa na kimataifa wa  kampuni ya VIP,pamoja na wafanyakazi wa Manispaa ya Bukoba mara baada ya kukagua na kutathmini eneo litakalotumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikubwa cha tiba ya Saratani,lililopo Makongo-Buhembe ,Manispaa Bukoba
 Katikati ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani ya matiti, Profesa Anthony Pais kutoka India na washauri wa  sheria ya kimataifa kutoka Marekani na Uholanzi ambao wameambatana na Fr. James Rugemalira katika ziara maalum ya kukagua eneo litakalo tumika kwa ajili ya Ujenzi wa kituo kikubwa cha tiba ya Saratani, Mjini Bukoba July 10,2015
Katikati ni  Daktari katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (MoI),  Prof.Joseph Kahamba katika picha ya pamoja na washauri wa kampuni ya uwekezaji ya VIP Engineering and Marketing Limited.
Mwanasheria wa Kampuni wa VIP Engineering and Marketing Limited  Bw.Respicious Didace pichani kushoto na Bi Joyce Kyobya wa VIP
Fr. James Rugemalira Mshauri wa kimataifa wa kujitegemea (International Independent Consultant) wa VIP Engineering and Marketing Limited akiendelea kukagua eneo hilo la Uwekezaji
Mwanahabari Mathias Byabato wa Channel Ten na Katibu Mtendaji KPC akiwajibika.
 Taswira jirani na eneo la ukanda wa uwekezaji wa kituo kikubwa cha tiba ya Saratani.
 Mr. Catres wa Manispaa Bukoba akitolea jambo ufafanuzi
Wakurugenzi wa Kampuni VIP Engineering and Marketing Limited Benedicta Rugemalira (kushoto)na Joe Mgaya (kulia)wakifuatilia ramani ya eneo la uwekezaji.katikati ni Mshauri wa VIP wa maswala ya mikakati Dr. Sako.
Wanasheria wa VIP Engineering and Marketing Limited wakikagua  eneo la mradi.
 Mkurugenzi wa Kampuni VIP Engineering and Marketing Limited akitoa utambulisho katika Mkutano wa Wafanyakazi wa Manispaa, Mkurugenzi na wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa Bukoba, July 10,2015
 Bi Joyce Kyobya na Bw. Ruta  Celestine wakiwa katika mkutano huo
Wadau wakipata chakula cha mchana mara baada ya shughuli ya kukagua eneo la uwekezaji
 Bw. Rahym Kabyemela  Mdau wa Kampuni ya uwekezaji ya VIP Engineering and Marketing Limited  akitolea jambo ufafanuzi.
 Mshauri wa mahusiano kwa umma Bi Secelela Balisidya wa VIP wakati wakiwasili mjini hapa.
Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd leo Julai 10,2015  imefanya ziara ya kutembelea eneo la Makongo ambalo litatumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Saratani mkoani Kagera. Mradi huo ambao una baraka zote za Manispaa ya Bukoba, unatarajiwa kutoa huduma si tu kwa nchi ya Tanzania, bali pia nchi za Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na nchi nyingine za jirani.

Akizungumza katika mkutano kati ya wafanyakazi wa manispaa ya Bukoba na washauri wa VIP, mshauri wa kimataifa wa kujitegemea wa VIP, Fr. James Rugemalira, ameushukuru uongozi wa manispaa ya Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla kwa kuridhia kutoa ardhi katika eneo la Makongo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo itakayojengwa na kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd.
Naye katibu tawala wa mkoa wa Kagera Bw .Nasoro Mnambila amesema kuwa Serikali imepokea ombi la VIP na hilo limejidhihirisha kwa uongozi wa mkoa kutoa ardhi hiyo na pia Serikali iko tayari kutoa ushirikiano kadri itakavyowezekana ili kufanikisha azma ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Kwa sasa mipango ya ujenzi wa hospitali hiyo iko katika hatua za awali na mshauri mkuu wa mradi huo, Profesa Anthony Pais kutoka nchini India amekuwa akitoa ushauri na ataendelea kutoa ushauri wa kitaalam katika hatua zote za ujenzi wa hospitali hiyo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau