Bukobawadau

LAWRENCE MASHA NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Lawarence Masha amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam kwa kosa la kutumia lugha ya matusi kinyume na sheria.

Baada ya kutuhumiwa kuvunja kifungu cha sheria namba 89 kifungu kidogo 1,A cha mwaka 2002 cha makosa ya jinai, Lawarence Masha aliwasili majira ya 10:40 chini ya ulinzi mkali.

Muda wote tangu alipowasili mahakamani hapo mahakama ilikuwa chini ya ulinzi mkali uliochagizwa na gari la maji ya washawasha.

Akisoma shitaka mbele ya hakimu mkuu mkazi wa mahakama ya Kisutu Dar es Salaam wariandere Lema, mwendesha mashitaka wa serikali Wankyo Simon ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo Agast 24 katika kituo cha polisi cha Ostabay alitumia lugha ya matusi ya wajinga nyie, washenzi hamna adabu na hamna dini matusi yaliyokuwa yakimlenga askali Juma Mashaka na wenzake, shitaka ambalo hata hivyo mtuhumiwa alikana na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili waliopaswa kusaini hati ya sh milioni moja kila mmoja ambapo suala la uhakikisha wa wadhamini hao lilishindwa kukamilika kwa wakati na mtuhumiwa akalazika kupelekwa gerezani Segerea.

Katika hatua nyingine watuhumiwa zaidi ya 19 wanaodaiwa ni wa kundi M4U wamefikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaki mawili yakiwemo ya kulanjama ya kutenda kosa la jinai na kufanya mkusanyiko uliokuwa na nia ya kufanya maandamano ambayo yangewafanya watu wa eneo la Moroko walipokuwa watuhumiwa hao kuwa na fikra za uwepo wa uvunjifu wa amani.

Hata hivyo kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na hakimu Emilius Mcharu  huku washitakiwa wakitetewa na wakili Peter Kibatala wamepelekewa Segerea baada ya uhakiki wa dhamana zao kuchelewa kwa muda wote ambapo kesi hizo zilipokuwa zikiunguruma mahakaamni hapo mahakaam ya Kisutu Dar es Salaam ilikuwa imezungukwa na ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama.
Next Post Previous Post
Bukobawadau