Bukobawadau

KUZUNGUMZA KWA DK SLAA NA MAONI YA WADAU MBALIMBALI

Baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa kuzungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam siku ya jana , Septemba Mosi, 2015, baada ya kimya kingi tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015 kupitia CHADEMA  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho amesema kuwa amejiondoa kwenye siasa na hatajiunga na chama kingine chochote cha siasa ila ataendelea kuwatumikia Watanzania kwa namna yoyote.

Dk Slaa ameamua kuvunja kimya na kutamka kuwa hakuwa likizo kama ilivyoelezwa, bali amejivua rasmi uanachama CHADEMA pamoja na Ukatibu Mkuu wa chama cha hicho, akisema sababu ya kufanya hayo ni kutokukubaliana wala kuridhishwa na mwenendo wa maamuzi na mambo yanayofanyika ndani ya CHADEMA.
MSIKILIZE DK SLAA KATIKA AUDIO HAPA CHINI

                      SEHEMU YA  KWANZA YA VIDEO:Hotuba ya Dr. Slaa alipojiuzulu Chadema & siasa SEHEMU YA PILI YA VIDEO DK SLAA AKIENDELEA KUFUNGUKA                                              SEHEMU YA MWISHO                                        Dk. Slaa amesema kuwa hakushiriki katika uamuzi wa kumkaribisha Edward Lowassa katika chama hicho kama ilivyodaiwa hapo awali bali aliletewa mapendekezo hayo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Alifafanua kuwa alihoji maswali mengi na kutaka majibu kama wangetaka akubaliane na mapendekezo yao. Suala kubwa alilohoji ni iwapo ujio wa Lowassa na watu wake ni mtaji kwa chama hicho au ni mzigo kwa chama hicho lakini hakupewa majibu. “Niliwauliza Lowassa anakuja kama mtaji au mzigo, yaani kwa lugha ya kiingeza ni asset au liability? Lakini suala la kwamba ni asset au liability hadi tarehe 27 hawakutuletea jibu,” alisema. Alieleza kuwa aliendelea kushikilia msimamo wake akiwataka waliokuwa wakipendekeza ampokee Lowassa akiwemo Askofu Gwajima ambaye alimtaja kama ‘mshenga’ kwenye mpango huo wa kumshawishi. Alisema baada ya viongozi hao wa Chadema kumshawishi kuwa Lowassa angekuja na timu kubwa ya wabunge 50 walioko madarakani hivi sasa kwa tiketi ya chadema pamoja na wakuu wa wilaya kadhaa, aliwataka wamletee majina yao pamoja na sharti la kuwataka kutangaza kuhama CCM kabla ya mchakato wa kura za maoni za kuwapata wabunge. “Niliwataka watuambie kama ni asset anakuja na nani, na wafuasi hao ni wa namna gani. Ni vijana wa mtaani, au anakuja na viongozi ambao ni serious ambao watatusaidia katika mapambano ya kweli?” Alisema hata hivyo walishindwa kufanya hivyo na kisha kuamua kushiriki mchakato wa kura za maoni huku wakihama baada ya majina yao kukatwa jambo ambalo amedai limefanya Chadema kuendelea kupokea ‘makapi’ ya CCM. Aliongeza kuwa hata wali0poanza kumtajia majina ya wachache walioamua kuhamia Chadema kutoka CCM aligundua kuwa ni makapi likiwemo jina moja la mtu anaeatajwa kuwa alikuwa kinara wa wizi wa kura CCM. Anasema kuwa hata kabla ya kuingia katia mkutano wa kamati kuu ambao Lowassa alishiriki, alifanya kikao cha awali na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Askofu Gwajima, kikao kilichodumu kwa muda wa saa tano (Kuanzia saa nne hadi saa tisa) bila mafanikio. “Tangu mwaka 2004 sikuwahi kutofautiana na mwenyekiti wangu katika kikao chochote cha chama, na hiyo ndio siri ya uimara wetu katika chama,” alisema. Kama kuna jambo tunatofautiana tulikuwa tunaitana tunaongea kabla ya kikao na tunakubaliana, lakini siku hiyo kwa mara ya kwanza kwenye kikao tulitofautiana. Dk. Slaa alieleza kuwa aliwahi kuandika barua ya kujiuzulu mara mbili lakini viongozi wa chama hicho walikataa kumkubalia na kumtaka kupumzika. Pia, aliwatuhumu viongozi wa chama hicho kuwa ni waongo kwa kuwa wamekuwa waliwadanganya wananchi hata pale picha zilipoonesha wako kwenye mkutano na Lowassa. Katika hatua nyingine, Slaa aliendelea kuweka msimamo wake kuwa Edward Lowassa alishiriki kwenye ufisadi wa Richmond na Dowans na kuwa yeye ndiye aliyekuwa ‘mastermind’ wa mchezo huo na vielelezo vinaonesha. Alitoa mfano wenye maneno makali kuhusu Chadema kumkaribisha Lowassa, akidai kuwa ni sawa na mtu kuchota ‘kinyesi’ kutoka chooni na kukihamishia chumbani kwako, huku akihoji kati ya chumba chako na kule ulikochota kinyesi ni wapi patakuwa choo. Alisema Lowassa ndiye kinara aliyelazimisha kampuni hewa la Richmond kupewa tenda ya kufua umeme wa dharura ingawa Tathmini ya Tenda ilionesha kuwa kati ya makampuni 8 yaliyofikia hatua ya tathmini, kampuni hiyo ilikosa vigezo na kupata marks 0. Kwamba alitumia uwaziri mkuu kuhakikisha wanapata tenda hiyo iliyoitia hasara kubwa serikali. Aidha, Dk. Slaa alisisitiza kuwa kamati Mwakyembe ilitoa ripoti ya kweli na kwamba yapo baadhi ya mambo ambayo hawakuyaweka wazi na vielelezo anavyo kwa kuwa vigogo 27 walihusika na wizi huo. Alimtaka Lowassa kujitokeza hadharani na kutaja kwa majina ya viongozi wa ngazi za juu anaodai kuwa walishinikiza kusainiwa kwa mkataba wa Richmond badala ya kuendelea kuwaficha. “Ajitokeze asema kwa majina hao viongozi wa ngazi za juu zaidi ya waziri mkuu ni nani na nani, aseme kwa majina kwa sababu waio juu ni Rais na makamu wa rais, nani aliyeelekeza? Amtaje,” alisema Dk. Slaa. Mwanasiasa huyo aliyesisitiza kuwa alikuwa anaongea ukweli mtupu muda wote, aliwataka wananchi kutoamini kile anachokisema waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye hivi sasa kwa kuwa yeye pia alishiriki katika ufisadi wa aina nyingine wakati wa serikali ya awamu ya tatu. Alimuita Sumaye kuwa ni kigeugeu kwa kuwa mwezi mmoja tu uliopita alitamka kuwa kama CCM ingempitisha Lowassa angehama chama hicho na kupinga uamuzi huo lakini leo ndiye anayempigia debe. Aliikosoa vikali hotuba ya Edward Lowassa ya kuwatoa gerezani Babu Seya na mwanae wanaotumikia kifungo jela kwa kosa la kuwalawiti watoto wadogo. Hakusita kuonesha uchungu aliokuwa nao kwa jinsi alivyoshiriki kwa nguvu yeye na mkewe Josephine katika kukijenga chama hicho lakini kimegeuka na kuwakaribisha wageni hao aliwaita makapi. Dk. Slaa alihitimisha kwa kutangaza rasmi kustaafu siasa za vyama na kueleza kuwa ataendelea kushiriki katika harakati za kulikomboa taifa bila kujihusisha na chama chochote cha siasa huku akimtaka Lowassa kujitokeza hadharani kujibu alichokisema na kwamba akifanya hivyo atamrudia tena na mengine ambayo hajayatoa hadharani. [Dar24.com na ziada unaweza kuisoma habarimasai.com]
MAONI MBALIMBALI BAADA YA KUJIUZURU KWA DK SLAA
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa facebook leo ameandika
Slaa hayupo kwenye karatasi ya kura. Naona watu wanahangaika na Slaa. Wengine tuliamua kukaa kimya kwani hekima inataka hivyo. Kwa kuwa watu wameamua kumtukana Dkt. Slaa ni lazima tutoke kulinda haki yake ya kusema yake. Tutatoka na tutaungana na Slaa kuwasema walio kwenye Ballot. Slaa hayupo kwenye Ballot. Mwacheni. Jadilini hoja zake sio kumjadili yeye. Eti hata watu wasio na rekodi yeyote ya kupambana na ufisadi nchi hii leo wanainua midomo yao kumsema Slaa. Mmeanza. Tutamsaidia Slaa, tutamaliza.
Sina mapenzi na Slaa. Alihusika kuniletea shida kubwa ya kisiasa nilipokuwa napigania MISINGI. Hata hivyo naipenda zaidi Tanzania kuliko tofauti zangu na Slaa. Ni lazima aheshimiwe na alindwe.
 Kupitia ukurasa wake wa facebook Ndugu  Bubelwa Kaiza ameandika:Nionavyo mimi:
1. Dk. Slaa ana hasira kali ya kutopewa fursa ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Dk. Slaa anafanya special assignment aliyopewa na CCM au pengine na wabaya wengine wa Bwn. Edward Lowasa, kuhakikisha mgombea huyo wa UKAWA hapewi ridhaa na wananchi kuongoza Jamhuri ya Muungno wa Tanzania. Mfanano wa approach na hoja zake na za makada wa CCM siyo coincidence.
3. Hoja zake zote (inawezekana ni kutokana na ujinga au upotoshaji wa makusudi) ni specifically personal and personally targeted dhidi ya Bwn. Edward Lowasa au campaign backup team yake; Bwn. Frederick Sumaye/Lawrence Marsha na wengineo.
4. Anajaribu kuaminisha umma kuwa yeye ndiye credible source ya jambo lolote analolisema au atakalosema kuwa ni kweli na sahihi.
5. Appeal yake ni preaching or sentimental presentation rather than scientific analysis ya siasa na utawala.
6. Kwa namna alivyomalizia wasilisho lake, in dhahiri kuwa ana lengo na mkakati wa muda wa kati kuendelela kutumia fursa ya Ukatibu Mkuu wa Chadema au fursa nyingine kama platform ya kushambulia mgombea uras wa UKAWA, akijitahidi kuaminisha umma juu ya kauli zake kuwa ni sahihi na ukweli mtupu.
7. Kuna kauli nyingi za uongo alizozitoa katika wasilisho lake, ikiwa ni pamoja na kusema kuwa hakuwahi kuwa na matamanio ya kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 Ndugu Evarist Chahali kuputia ukurasa wake wa facebook anasema ;Ni vigumu kumridhisha mwanadamu. Actually, ukitaka kuwa na wakati mgumu maishani, hangaika kuridhisha wanadamu badala ya kuridhisha nafsi yako. Dkt Slaa alipoamua kukaa kimya aliitwa kila jina: from mnafiki to mpenda madaraka. Leo kaitikia wito wa waliomtaka asikae kimya tu na kueleza yake ya moyoni, bado anaandamwa na kuitwa kila jina baya: from mnafiki to mpenda madaraka. The good news is, ukweli una tabia moja kuu: "ukweli siku zote hubaki kuwa ukweli. Kuuchukia ukweli hakuubadili kuwa uongo." Pia ukweli una tabia nyingine muhimu: "ukweli huuma (truth hurts)." Laiti wanaomkejeli Dkt Slaa wasingekuwa wanaumizwa na alichoongea leo, wangempuuza kama wanavyopuuza kauli nyingine dhidi yao. La muhimu ni hili: TRUTH SHALL SET YOU FREE (ALTHOUGH IT WILL FIRSTLY HURT YOU).
 Happy September!
Tindu Lissu akihojiwa na redio redio VOA Swahili station Mh.Lissu anasema ameshangaa sana maneno aliyoyasema leo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Anasema Dr.Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi January na mwezi April akathibitishwa na kamati kuu,
Anaendelea kusema ameshangaa Dr.Slaa kusema Gwajima ndo alimleta Lowassa jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dr. Slaa mwezi wa tano ndo alianza kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima

Anasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.

Anasema dr. slaa asiwadanganye watanzania tatizo ni urais na mchumba wake.
Anasema ameacha siasa tangu siku ya kikao cha kamati kuu alipoandika barua ya kujiudhuru kwa nini amepokea mshahara wa mwezi huu?? kwanini anaendelea kutumia gari la chama la katibu mkuu na nyumba aliyonunuliwa na chama muulizeni awaambie kwanini anaendelea kunufaika na hayo yote toka CHADEMA??
Next Post Previous Post
Bukobawadau