Bukobawadau

UJUMBE WANGU KWA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA KATIKA KUELEKEA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI MKUU OCTOBER 25


Lucy Patrick
Kalamu yangu mdomo wangu leo nataka nizungumze na wanahabari wenzangu waandishi na wataangazaji pia nataka mjue kwambaa karama hii au kipaji hiki tumepewa sio kwamba sisi tulistahili sana kuliko wengine hapana  ni kwamba tuliaminiwa kwamba tunaweza kutumia midomo yetu na kalamu zetu katika kusema na kuandika ukweli ili tuweze kuelimisha,kutoa habari na hata kuburudisha ikiwezeekana naomba niwashauri tutumie karama zetu vizuri tuache ushabiki ambao hautakuwa na manufaa yeyote kwa taifa letu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi maana naona tumeacha maadili ya kazi yetu na sisi tumetekewa na ushabiki bila kujiuliza kuwa kwa kufanya hivyo hatuisaidii nchi yetu.Tuache ushabiki turudi kwenye kazi yetu tufanye tafiti tuhoji kuhusu sifa za kiongozi  bora ambaye tunamtaka tuwaambie wananchi ili wao wawapime na kuchuja kama sera zao  zinafaa sio na sisi tunakumbwa na upeo hii ni mbaya tuache tuwaambie ukweli vijana wanaoimba mabadiliko kila siku waamini kwamba mabadiliko yanaanza nawao wenyewe kubadilika na kubadiliha fikra zao na mitazamo kwamba maendeleo yanaletwa na mtu mmoja hilo ni hapana nataka wajue maendeleo yanaletwa na jitihada zao wenyewe kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo ukweli ni kwamba hakuna hata kiongozi mmoja ambaye anaweza kugawa maendeleo kwa kila nyumba tuwaambie maendeleo yanaletwa kwa jitihada na mipango thabiti  wanachotakiwa kufanya ni kuchagua kiongozi safi na thabiti mwenye sifa za uongozi anayeweza kutengeneza mfumo mzuri utakao wawezesha kufanya kazi zao kwa amani na utulivu pasipo mvurugano na mwisho wa siku wakafikia malengo yao pamoja na kwamba ni kweli tunahitaji mtu mwenye kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu.Inaniuma sana kuona kila siku  vijana wanadanganywa tu wataletewa ajira na maendeleo wakati ukweli hata tukiangalia nchi zilizoendelea hakuna mtu anayeletewa ajira nyumbani ni pale tu kijana anapokuwa anajitambua na kuweka malengo katika maisha yake na kuacha kubweteka na kufanya kazi kwa bidiiiwe ameajiriwa au amejiajiri hakuna shortcut katika maisha waandishi  tufanye tafiti kwa nchi zilizoendelea wao waliwezaje kujikwamua na changamoto kama zetu ili tuisaidie jamii yetu tusiegemee upande mmoja penye kusifia tusifie na penye makosa tukosoe tu bila kumuogopa mtu wala chama tuangalie viongozi bora na sio tuseme huyu ni kiongozi bora sababu mtu Fulani kasema hapana tuzungumze nao tufanye mahojiano nao maana nafasi hiyo tunayo tukae nao karibu tuhoji kiundani  ikibidi tuangalie historia zao majimbo yao  tulinganishe na maneno yao vinaendena na sio tusema huyu hafai sababu nanihii kasema hapana tufanyeni kazi wapendwa tena kwa uadilifu bila kupendelea chama chochoteau mtu yeyote ni hayo tu kwa leo mwisho nasema hivi mwandishi tuaache ushabiki  turudi kwenye misingi ya kazi zetu tutumie kalamu zetu vizuri ili kuleta mabadiliko chanya katika nchi yetu atakaye tegua vitendawili na maswali mengi au mkanganyiko kwa wananchi ni sisi kama tutatumia vizuri kalamu zetu na karama zetu..MUNGU IBARIKI TANZANIA. 


HAPA NI BAADHI YA COMENT ZA  WATU WANAVYOTUTAZAMA WAANDISHI

 • Roger Magoha true say shikamoooo
 • Lucy Patrick asante kwa kusoma ndugu mtangazaji Idrissa da Silencer
 • Idrissa da Silencer Aku mie kanjanja tyuuuuu Lucy Patrick
  Unlike · Reply · 1 · 32 mins
 • Briane Muhongo Good idea Lucy
  Unlike · Reply · 1 · 29 mins
 • Moses Ng'wat Lucy hayo unayoyaona kwa waandishi ni matokeo ya tatizo la msingi lililopo katika media zetu, huwezi kutafuta usawa na umakini wa mwandishi huku chombo anachofanyia kikiwa kinamilikiwa kwa asilimia 70 na mwanasiasa anayeegemea upande fulani.

  Hebu fikiria hii, chombo fulani bodi yake yote inawajumbe ambao ni wanasoasa tena wa mlengo fulani
  Unlike · Reply · 1 · 28 mins
  • Lucy Patrick ni sawa ndugu mwandishi lakini wewe lazima usimamie ukweli na haki hilo tulitakufanya uwe wewe bila kujali chombo ni cha mlengo upi na wananchi na jamii itakupa heshima iliyotukuka kwa hilo
 • Raphael Manga Dadangu Lucy Patrick umenena vyema kwa hilo maana nyie kama waandishi wa habari mnanafasi kubwa ya kuijenga nchi au kuibomoa nashukuru kuona wewe dadangu ni miongoni mwa wanahabari mnao jitambua,
  Kunakitu nimekiona kwa miongoni pia kwa vyombo vya haba
  ...See More
  Unlike · Reply · 1 · 28 mins
 • Justin Minoti Jr. Dada kunywa supu hapo na azam cola nakuja kulipa
  Unlike · Reply · 1 · 24 mins
 • Hamisi Halfani Shembaruku Wastahili pongezi kwakuliona hilo wasije tuletea janga kwakusambaza chuki na ubinafsi kati mwishowe amani tuliyo nayo itoweke.
  Unlike · Reply · 1 · 23 mins
 • Lusekelo Mtafya Kuchafuka na kwa waandishi wahabali chanzo chake niumasikini waandishi wahabali kipato chao kidogo ko asilimia kubwa wananunuliwa na hii yote inatoana na kukosa uzalendo mtu anataka akianza kazi miaka michache anunue gali ajenge nyumba aonekane mtaani kama yupo sasa mambo gani na ikione kana kunachombo cha habali kinatoa taarifa sahihi zinazo pingana na mfumo tuliopo saizi kinachunguzwa nakutafutiwa sababu zisizo Rasimi kitafungiwa tu

  • Emilly Lazarius Sahihi mama
  • Omary Mandia Jambo lamsingi umelisema dada,cku zote machafuko huchochewa zaidi na wanahabari,na kiukweli msipo badilika nchi hii itakua pabaya november,kwani walowengi hutumia kalamu zao kuchambua ushabiki wao ambao hujaza sumu kwa wananchi jambo ambalo ni hatar mno.

  Imeandaliwa na  http://lucypatrickwatz.blogspot.com/
Next Post Previous Post
Bukobawadau