Bukobawadau

MAGUFULI ALIVYOTIKISA MJINI TABORA LEO

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote. 
PICHA NA MICHUZI JR-TABORA

 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
 Mmoja wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.


 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.

 Wananchi wakishangilia .
  Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Simiyu wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli kuwahutubia akitokea wilayani Nzega mapema leo mchana
 Wafuasi wa chama cha CCM sambamba na wananchi wa Uyui wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
 Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa na Mabango yao ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,wakimpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassani Wakasubi akitoa ufafanuzi mfupi kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
  Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
 Wananchi wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Next Post Previous Post
Bukobawadau