Bukobawadau

MASWALI YA WIKIENDA KISIASA

Maswali ya Wikienda:NA Mimi Mwanakijiji

A. Ni lazima kwa kila MwanaCHADEMA - mwanachama, mfuasi au shabiki - kumkubali na kumpigia kura Lowassa kuwa Rais? Je, mtu huyo akiwa na sababu za kutompigia kura Lowassa afanye nini? Inawezekana awepo mtu kama huyo kweli CDM?

B. Ni lazima kwa kila Mwana CCM - mwanachama, mfuasi, au shabiki - kumkubali na kumpigia kura Magufuli kuwa Rais? Je, mtu huyo akiwa na sababu za kutompigia kura Magufuli afanye nini? Inawezekana awepo mtu kama huyo kweli CCM?

C. Unafikiri ni chama gani kina watu wengi wenye mwelekeo unaopingana na pendekezo la chama chao? Hasa ukizingatia kuwa kila chama kinategemea kura za wanachama wake kwanza kabisa na zaidi kuliko kura za kundi jingine lolote?

D. Unafikiri wana CCM ambao hawakufurahia Lowassa kukatwa jina lake na wakapewa Magufuli kuwa mgombea wao (rejea "tuna Imani na Lowassa") ni wengi zaidi kuliko wana CDM ambao hawakufurahia Slaa kukatwa na wakapewa Lowassa?

NB: Si lazima ujibu maswali kama ni magumu au hayaeleweki au huyapendi au yanakera sababu ya mwulizaji. Unaweza kufanya jingine lolote badala ya kujibu maswali - kama kutoa maoni mengine yasiyo jibu maswali.
Next Post Previous Post
Bukobawadau