Naaam!Waswahili wanasema Nyota njema huonekana asubuhi ,Msemo huu ni sawa na ule wa kihaya maarufu usemao kwamba ''Obulanula bubanza ne'nanga"hii imedhihili wakati Bwana Smart Petro Baitani akizindua rasmi kampani za kuusaka Udiwani kwa manufaa ya wananchi wa Kata ya Kagombo Mjini Bukoba jioni ya leo Jumamosi Oct 3,2015.
Sehemu ya wananchi na wanaCCM waliohudhuria mkutano wa Kampeni wa Mgombea Udiwani wa Kata ya Kagondo Bwana Smart Petro Baitani.
Balozi Khamis Kagashiki akizungumza na wananchi na kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni wa Mgombea Udiwani Kata Kagondo.
Bwana Smart Baitani Upana wa wigo wa mtandao alionao unadhihirisha ukomavu wa akili yake, na
kwamba fikra zake hazikufungika ndani ya Kata ya Kagondo na Mji wa
Bukoba bali zimevuka ziwa Victoria na kuangaza nje na ndani ya nchi
mpaka bara ya Amerika .
Umati wa watu ukiesikiliza kwa makini
na kuyatafakari manene ya Balozi Khamis Kagasheki wakati akizungumza
katika Mkutano huo.
Bi Mwajabu Galiatano akimnadi na kumuombea kura Bwana Smart Baitani
BUKOBAWADAU MEDIA tunaendelea kujitahidi kuripoti kampeni za uchaguzi
kama sehemu ya majukumu yetu ya kila siku kuhakikisha wananchi wanapata
habari. Pia tunatoa wito kwa Wagombea wa vyama mbalimbali wajitahidi
kutushirikisha ikibidi na kuchangia gharama za uendeshaji ..!
Ndugu Jamal Kalumuna na Ndugu Samora Lyakurwa wakiwasili katika mkutano huo
Burudani maalum kutoka kwa wasanii maalum zikiendelea kuupamba uzinduzi huo
Baadhi ya Wanawake wa Kata ya Kagondo waliojitoa kimasomaso kumuunga mkono Bwana Smart Baitani katika harakati za kuisaka Kagondo mpya
Kijana Amani Kabuga akifuatilia kinachojiri katika mkutano huo
Taswira mbalimbali katika mkutano huo
Shangazi yake Mgombea Ndugu Smart Baitani akitoa neno katika mkutano huo
Utapata kumsikiliza na kutazama katika Sehemu ya Video hapa Chini Bwana Smart Baitani na WanaKagondo Kwa ulimi wa fasaha kuliko wa Karama.
Mdau Benard Matungwa akitolea jambo ufafanuzi
PITIA SEHEMU YA MKUTANO HUO KATIKA VIDEO HAPA CHINI
BUKOBAWADAU MEDIA tunaendelea kujitahidi kuripoti kampeni za uchaguzi kama sehemu ya majukumu yetu ya kila siku kuhakikisha wananchi wanapata habari. Pia tunatoa wito kwa Wagombea wa vyama mbalimbali wajitahidi kutushirikisha ikibidi na kuchangia gharama za uendeshaji ..!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Shukrani za dhati wana Bukoba wadau media kwa shughuli zenu nzuri wagombea wetu wanaweza sana na wana hoja za msingi sio kama wale wanaotumika kupanda majukwaa kumsema Swaiba wetu
Post a Comment