JIJI LA MBEYA HATARI KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
Wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiendelea na shughuli zao kama kawaida . |
Na
Mwandishi wetu,Mbeya
Halmashauri
ya jiji la Mbeya limewataka wafanyabiashara ndogondogo hususani wa
chakula kujijengea tabia ya kuchoma taka nyakati za jioni mara wamalizapo
kuuza biashara zao na si kusubili gari ya taka kuja kuzoa.
Aidha
imewataka wakazi hao kuondokana na fikra
duni ya kuamini kuwa kazi ya uzoaji wa taka na kusafisha mazingira ni ya
halmashauri ya Jiji na sio mali ya mtu.
Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Lazaro, amesema,
wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi na sio kusubili kupigizana kelele na
serikali kwa kuwahimiza kufanya usafi kwani adui mkubwa wa afya ni uchafu hivyo
kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwezake katika kutunza mazingira.
Hali hiyo
imesababisha kuwepo kwa malimbikizo mengi ya taka kwenye sehemu
zisizorasmi ndani ya JIji la Mbeya na kupelekea jiji hilo kuwa chafu
hususani katika maeneo ya sokoni.
Amesema,
hivi sasa halmashauri ilianzisha mpango wa uzoaji wa taka barabarani ambapo
mpango huo umeonekana kupokelewa na wananchi kwa asilimia 100 changamoto
inakuja kwa upande wa halmashauri kuonekana kuzidiwa kutokana na ukosefu wa
vitendea kazi.
“Halmashauri
ilianzisha zoezi la kupitia taka zinazozalishwa na wananchi ambazo huziweka
barabarani na magari yanapitia lakini mapango huu umeonekana kuzaa matunda kwa
jamii kuupokea lakini tatizo ni uhaba wa vitendea kazi,”alisema.
Alisema,
ili zoezi hilo lifanikiwe halmashauri inahitaji zaidi ya gari saba za ubebaji
taka na kontena 80 lakini mpaka sasa magari yaliyopo ni manne na kontena 30 .
Hata hivyo
kutokana na changamoto hiyo, Lazaro anawasihi wananchi kujenga tabia ya kuweka
mazingira safi hasa kipindi hiki cha mvua kwani ndipo magonjwa ya mlipuko kama
kipindupindu yanapoibuka na kusababisha vifo vya watu.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG MBEYA