Rais Magufuli asaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa na awasili Mjini Dodoma kwa Gari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo Ubalozini hapo.
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi
130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini
Paris, Ufaransa.
Pamoja na kutia
saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa
Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na
ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu
Dokta Magufuli
ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema
Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki
kigumu cha majonzi.
Aidha Rais
Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze
kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku
Katika hatua
nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli
amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
Mheshimiwa
Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya
shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa
na;
Gerson
Msigwa
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November
17, 2015