Bukobawadau

UZINDUZI WA KAPOTIVE YOUNG SITERS

Kapotive Singers- Bukoba
Mpendwa, tunayo furaha kukufahamisha kuwa Jumapili, tar. 29/11/2015 tutakuwa na uzinduzi wa kikundi chetu kipya cha KAPOTIVE YOUNG STARS. Kikundi hiki kinaundwa na vijana wa utamadunisho cha Mt. Theresia wa Mtoto Yesu Parokia ya Bukoba, ambao wanaimba na kucheza nyimbo zetu kwa umahiri mkubwa.
Ili kuwezesha maandalizi ya siku hiyo, kiingilio kitakuwa kama ifuatavyo:
- Watoto 2,000.
- Wakubwa 5,000.
- VIP 10,000.
Sehemu kubwa ya mapato ya siku hiyo itasaidia kuwanunulia watoto wenyewe mahitaji ya shule kama sare, viatu, daftari, begi n.k

Shughuli hii itafanyika katika ukumbi wa Rumuli kuanzia saa 9 jioni. Watasindikizwa na kikosi kizima cha KAPOTIVE Star Singers.
Karibuni sana tuwaunge watoto wetu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau