Bukobawadau

KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI MH. WILFRED LWAKATARE

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mh.Wilfred Lwakatare 'Lwaks' anapenda kutumia fursa hii kuwakaribisha WanaKagera,Wapenda Maendeleo na Wadau wa Bukoba Mjini katika Kongamano la (Bukoba Municipal Developmental Conference-BUMUDECO) litakalojadili fursa na changamoto za Bukoba Manispaa na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe Tarehe 27 Disemba, 2015
Muda: Kuanzia Saa 9:00 Alasiri
Mahali: Bukoba Mjini (Utajulishwa ukumbi)
Wanakagera wote mnakaribishwa kuijenga Bukoba!
#‎MabadilikoNiSasa‬ #‎Elimu‬

Pichani kulia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Mh.Wilfred Lwakatare 'Lwaks'(katikati ) alipofika ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada kuchaguliwa na kuapishwa kwake.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella akiongoza kikao kidogo kilichofanyika ofisi kwake
Pichani katikati niMhe. Chief Karumuna  aliyesimamishwa na UKAWA kama mgombea wake wa Umeya katika uchaguzi wa Mayor Bukoba Manispaa utakaofanyika siku ya Ijumaa Disemba 11,2015
 Mh Ibrahimu Idd Mabrouk Diwani Kata ya Bilele
 Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Mh.John Mongella mazungumzo yakiendelea na viongozi wa Ukawa Jimbo la Bukoba Mjini.
 Mbunge wa (Viti Maalum,Kagera CUF) Mh.Savelina Slivanus Mwijage akiagana na Mkuu wa Mkoa Mh.John Mongella SEHEMU YA VIDEO MH LWAKATARE AREJEA JIMBONI NA KUKUTANA NA RC
Next Post Previous Post
Bukobawadau