Bukobawadau

KAGERA WAASWA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI ILI KUKUZA UCHUMI WA MKOA NA TAIFA KUPITA SEKTA ZA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage asistiza kumalizwa kwa migogoro ya ardhi kwa maridhiano bila kupelekana mahakamani kati ya wananchi na wawekezaji ili kukuza sekta za viwanda na biashara na kuinua uchumi wa mkoa  wa Kagera wenye fursa nyingi za uwekezaji  hasa katika sekta za viwanda na biasahara.
 Waziri Mwijage aliyasema hayo katika majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera aliyoifanya tarehe 04 hadi 05.01.2016 ambapo alitembelea  viwanda vya Vickfish,TANICA, Hamir Hamza Tanzania Ltd vilivyopo katika Manispaa ya Bukoba. Vilevile Waziri Mwijage alivitembelea viwanda vya Kagera Tea Company Ltd, Kagera Fish katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba alitembelea shamba la chai la Binengo Izigo na alimalizia ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa kutembelea kiwanda cha Kagera Sukari na eneo lilotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya viwanda (Export Processing Zone, EPZ) lililopo Omukajunguti lenye hekta 3000.
Dhumuni la kutembelea viwanda hivyo Waziri Mwijage lisema ni kuhakikisha vinafanya kazi ipasavyo kwa kiwango serikali ilichokusudia na kuhakikisha asilimia 40% ya Watanzania ambao ni nguvu kazi wanafanya kazi katika viwanda na kuzalisha kwa wingi ili viwanda hivyo viweze kuchangia katika pato la taifa kwa asilimia 15% ifikapo  mwaka 2020
Kuhakikisha Watanzania waliopo katika sekta ya viwanda wanafanya kazi wanazotakiwa kuzifanya kwa kujifunza teknolojia mpya badala ya kuendelea kuwategemea wataalam kutoka nje tu. Viwanda kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa  kuhakikisha waajiliwa wanapewa stahiki na haki zao bila migogoro yoyote ile wawapo kazini.

Kuhakikisha Watanzania waliopo katika sekta ya viwanda wanafanya kazi wanazotakiwa kuzifanya kwa kujifunza teknolojia mpya badala ya kuendelea kuwategemea wataalam kutoka nje tu. Viwanda kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa  kuhakikisha waajiliwa wanapewa stahiki na haki zao bila migogoro yoyote ile wawapo kazini.

Waziri Mwijage kwa  kutoa wigo mpana katika  sekta ya uwekezaji hasa  viwanda aliagiza kila Halmashauri nchini kuhakikisha  zinatenga maeneo ya kujenga au kuanzisha mitaa ya SIDO ili  kutoa fursa kwa wajasiliamali wadogowadogo kufanya shughuli zao  katika eneo moja lilotengwa na kujengwa au kugawanywa kitaalamu na wataalam kutoka katika Wizara yake ambao wako tayari kufanya kazi hiyo.
 Nao wadau wa uwekezaji hasa wafugaji wanaofuga kisasa waliohudhulia kikao  cha majumuisho cha Waziri Mwijage waliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwamilikisha ardhi au vitalu wanavyovimiliki kwa kuwapatia hati kamili badala ya kupangishwa na NARCO ili waweze kukopa na kuendeleza ufugaji wa kisasa zaidi, aidha serikali kuwa inatoa majibu kwa wakati na haraka kwenye masuala ya kukuza uchumi wa nchi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau