Bukobawadau

MKUTANO MKUU WA KADEA JAN 5,2016

Meza kuu wakiongozwa kuimba wimbo maalum wa KADE(ndi wa KADEA akala na kalenge)
 Viongozi wakuu wa KADEA
 Mwenyekiti,Enock Kamuzora akiwasilisha taarifa yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo mkuu
MKUTANO mkuu wa shirika la maendeleo ya wananchi wa Kata za Kanyigo na Kashenye-KADEA  kwa mwaka 2015,umefanyika 05 Januari mwaka huu,pamoja na mambo mengine ,umeazimia kuendelea kuchangia mfuko wake wa elimu kwa ajili ya kuinua elimu katika shule za msingi kwa kata hizo mbili.

Mfuko huo wa elimu ulioanzishwa mwaka 2012 umesaidia kupandisha kiwango cha ufaulu kutoka wanafunzi 400 hadi zaidi ya wanafunzi 400 wanaojiunga na sekondari sasa.

Mwenyekiti wa KADEA,Enock Kamuzora,akiwasilisha ripoti yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu,alisema mwaka 2015 Mei, mtihani wa mock wa Mkoa wa Kagera kwa darasa la saba,kwa kata ishirini za Wilaya ya Missenyi,Kata Kanyigo ilishika nafasi ya kwanza na Kashenye nafasi ya pili.

Katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba wa mwezi Septemba mwaka jana,Wilaya ya Missenyi,Kata Kanyigo ilikuwa ya kwanza na Kashenye ya tatu.
Aidha kwa miaka mitatu mfululizo,katika shule ya sekondari Kanyigo,inayomilikiwa na shirika hilo,hakuna mwanafuzi yeyote aliyefeli katika mitihani ya Taifa ya kidato cha pili,nne na sita.
Next Post Previous Post
Bukobawadau