SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

03 February 2016

KOO ZA BUHAYA, TAMADUNI NA MIIKO

Koo, tamaduni na miiko katika Buhaya ni vitu ambavyo vinatambulika na vina maana sana katika kumwelezea mtu husika katika mambo mbali mbali ya kijamii katika Buhaya.
Mambo haya yameanza kupotea, mbaya zaidi vijana wengi hawajapata fursa ya kufahamu haya mambo na wengine kushindwa kabisa hata kufahamu koo zao kutokana na sababu mbali mbali.
BUKOBAWADAU MEDIA inatumia jukwaa lake kuangazia mambo mbali mbali ya koo ili kuwapa mwanya vijana kufahamu kwa kina mambo haya.

Kwa kuanza; kika mtu ataje ukoo wake ili tujue ni koo ipi inawatu wengi zaidi na Tutakua tukijadili ukoo mmoja mmoja, na ukoo wenye watu wengi zaidi ndio tutaanza nao
Inasemekana kuwa wahaya walitokea Misri na kupitia Uganda na hatimaye kuanza maisha katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania
Wakati wamishenari wa Ulaya walipowasili, eneo hilo lilikuwa maarufu kwa kuwa na Kadinali wa kwanza wa kikatoliki marehemu Laurian Rugambwa.

Aidha watu wa Jamii hii walizingatia sana elimu ikilinganishwa na makabila mengine nchini Tanzania
Kabla ya kuwa na serikali ya taifa watemi ndio walitambuliwa kama wakuu wa jamii ya Wahaya.
Ndoa ni swala linaloheshimiwa katika kila jamii, na ni jambo linaloenziwa sana na jamii ya Wahaya.
Mahari ya Ng'ombe ama mbuzi ilitolewa kwa baba wa msichana kulingana na makubaliano ya pande zote mbili.
Wahaya wana koo 8 ambazo ni Bumbira, Edangabo, Ganda-Kiaka, Hamba, Hangiro, Mwani, Nyakisisa, Ekiziba na Yoza.

Ni wazi kuwa jamii ya wahaya ni watu waliojitambua mapema.Sifa na utamaduni wetu ni muhimu kuvitunza kwa manufaa ya sasa na baadae.Kushindwa kuenzi vitu hivyo ,vizazi vijavyo vitakuwa watumwa wa jamii na tamaduni nyingine.
Hivyo mdau msomaji toa maoni yako tueleze unatoka Ukoo gani (Oluganda )sifa za ukoo huo na miiko yake na chochote unachokijua kuhusu ukoo fulani..

Kumbuka ku like na kushare ukurasa wetu wa Bukobawadau Entertainment Media

5 comment:

Anonymous said...

Mimi ukoo wangu ni Mrwanikazi, Miiko ya Warwani ni Ente ya Runya (ngombe mwenye mabaka kama chui) Muzimu wetu ni Chui ambae anaitwa Kiaano.

Asanteni.

Unknown said...

Safi sanaa, ila sijaona ukoo wa abasizi

Unknown said...

Tunanze na ekiziba

Abu_Nurayda said...

Umesahau abankango, hawa ni wajomba zangu na mtemi wao ndiye yule wa KABALE KANGAIZA

Unknown said...

Mbanze mbabaze, inywe nimufumoola lulimi ki kushaaga Oluhaya lwaanyu? Mumanye okwo Kabaale k'Omukama kaataine Katoma. Nimwo Omukama Rukamba II yataiize 2007. Kandi Kabaale kali aka Ngaiza kaataine Maruku. Ka olikwenda oluganda lwaawe kalutondwa, obanze kweetonda iwe wenka nilwo abandi balaaluga nyuma bakakutonda.

You have to master your own mother tongue before jumping to other languages. Loosing the prime personal identity is just selling yourself to slavery.

Ndugu zangu, tusidanganyike. Kiwahili hatukiwezi, kama wewe unakiweza mbona ukikitamka mtu anakutambua haraka kuwa wewe ni Muhaya? Kunguru alisema, "Kila mtu kwaaao, kwaaao."

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU