Bukobawadau

BALOZI DR KAMALA AENDELEZA ZIARA KWA KUTEMBELEA VYUO VYA UFUNDI VYA PARTAGE

Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ufundi Byayungu kilichopo Kanyigo-Missenyi Bwana Deusidedith Mwijage pichani kushoto wakati akiwa katika ziara ya kutembelea Vyuo mbalimbali vya Ufundi vilivyomo ndani ya Jimbo lake.
Balozi Dk. Diodorus Kamala kwa kutambua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Wilaya ya Missenyi na Taifa  kwa ujumla, ameamua kufanya ziara katika vyuo vya Ufundi  ili kuona ni namna gani ataweza kusaidia vijana, hii ni katika kutekeleza Ilani yake mpango  mpango wa kupeleka vijana kumi (10) kutoka kila Kijiji kuwapeleka katika Vyuo mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia mafunzo maalumu.
 Hii inatokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia tisini 90% ya Vijana wanaomaliza kidato cha nne Wilayani Missenyi hawapati nafasi ya kuendelea na elimu ya juu. Mpango huo utasaidia kutengeneza ajira,kukuza kipato,kuandaa mifano (models) kwa vijana wenzao, kupunguza uhalifu, ulevi,vijiwe n.k


 Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala ametoa wito kwa wananchi wa Missenyi kutowaacha vijana wao waliomaliza Elimu ya Msingi na Kidato cha nne bila msaada na badala yake kuwapeleka vyuo vya ufundi ili waweze kujiajiri.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Bwoki
 Balozi Dk. Diodorus Kamala akipata maelezo kutoka kwa Makamu wa Chuo cha  Partage cha Bwoki Mwl.Zamda Mohamed alipotembelea Chuo hicho kinachotoa mafunzo mbalimbali
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza kwa makini Mwalimu wa Ufumaji Benitha Johnson pichani kushoto wakati  mwanafunzi Lilian  Mjongo akiendelea akidalizi. 
 Balozi Kamala amehaidi kusomesha Vijana Kumi kutoka kila Kijiji ndani ya Jimbo la Nkenge katika Vyuo mbalimbali vya Ufundi kwa nia ya kuwawezesha kujiajiri na kuongeza kasi ya kupambana na umasikini. Jimbo la Nkenge lina vijiji 75. 
 Mkurugenzi wa Elimu Shirika la Partage, Theodory Kaiyuzi akitolea jambo Ufafanuzi kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala wakati wa ziara yake Chuoni hapo
 St .Dinna Nkondo pichani kushoto wakati akitoa neno la Shukrani kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala kutembelea Chuo hicho
 Baadhi ya walimu wa Chuo cha Ufundi cha Partage kilichopo Bwoki Wilayani Missenyi

KWA UJUMLA ZIARA YA MH BALOZI DR. DIODORUS BUBERWA KAMALA JIMBONI NKENGE 

Mh Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala alifanya ziara jimboni kwake Nkenge kwaajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa kipindi cha miaka mitano, pia kwa kumchagua kwa kura nyingi Mh John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuwachagua madiwani wa chama cha mapinduzi. Vile vile Mh Balozi Kamala alitumia fursa hiyo kuongea na wananchi katika kata zote zilizoko jimboni Nkenge ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuangalia jinsi ya kuzitatua. Ziara hiyo ilimfikisha Mh Balozi Kamala katika vijiji vyote vilivyoko katika jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi.
 Katika zira hiyo iliyodumu kipindi cha wiki mbili, Mh Balozi Kamala alitembelea shule mbalimbali jimboni ili kujionea mwenyewe utekelezaji wa Sera ya Elimu Bure. Mh Balozi Kamala alitumia fursa hiyo kuongea na walimu wa kuu wa shule za msingi na sekondari kujua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa Sera ya Elimu Bure. Matatizo mbalimbali yaliweza kuibuliwa na walimu hususani uchakavu wa miundo mbinu mfano vyumba vya madarasa, uhaba wa madawati n.k. Mh. Balozi Kamala katika kuunga mkono jitihada za Mh Rais Magufuli, Mh mbunge alichangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule jimboni Nkenge.
Vilevile Mh Balozi Kamala alitembelea vyuo vya ufundi stadi wilayani Missenyi vinavyosimamiwa na shirika la Partage ili kujua jinsi vinavyofanya kazi. Lengo hasa la kutembelea vyuo hivi kwa mujibu wa maelezo ya Mh. Balozi Kamala, ni kuhakikisha anapata vijana kumi kila kata ambao atawasomesha katika vyuo hivi ili baadae waweze kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali za ufundi.
Balozi Kamala pia alichangia michango mbalimbali hususani kwenye sekta ya michezo ambapo alitoa jezi, mipira na fedha taslimu kwa timu mbalimbali za kata jimboni Nkenge ili ziweze kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Mh Balozi Kamala alitumia fursa hii kuwataka wananchi kufanya kazi kiwa bidii ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU. Aliwataka wananchi katika vijiji mbalimbali kutokuendekeza unywaji pombe uliokithiri hasa nyakati za kazi. Aliwaagiza madiwani wote kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi.
 Mwisho Mh Balozi Kamala alitembelea vyuo vya ufundi stadi wilayani Missenyi vinavyosimamiwa na shirika la Partage ili kujua jinsi vinavyofanya kazi. Lengo hasa la kutembelea vyuo hivi kwa mujibu wa maelezo ya Mh. Balozi Kamala, ni kuhakikisha anapata vijana kumi kila kata ambao atawasomesha katika vyuo hivi ili baadae waweze kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali za ufundi.

Balozi Kamala pia alichangia michango mbalimbali hususani kwenye sekta ya michezo ambapo alitoa jezi, mipira na fedha taslimu kwa timu mbalimbali za kata jimboni Nkenge ili ziweze kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Mh Balozi Kamala alitumia fursa hii kuwataka wananchi kufanya kazi kiwa bidii ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU. Aliwataka wananchi katika vijiji mbalimbali kutokuendekeza unywaji pombe uliokithiri hasa nyakati za kazi. Aliwaagiza madiwani wote kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau