Bukobawadau

HAFLA YA KUMPONGEZA MWL PELAGIA PHILBERT KWA KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA YAFANA NYUMBANI KIJIJINI GERA KASHAMBYA !

Matukio ya picha yaliyojiri katika hafla fupi iliyo andaliwa na Familia ya Mwl.Philbert F. Byabato wa Kijijini Gera kwa ajili ya kumpongeza mwanafamilia wao Mwl. Pelagia Philbert ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma baada ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake na miaka 40 ya Utumishi.

Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Ibada iliyoongozwa na Fr. Godwin Rugambwa pichani imefanyika Nyumbani kwao Kijijini Kashambya -Gera mwanzoni Jumatatu ya Pasaka March 28,2016.


Wakati Ibada hii ya kumpongeza Mwl. Pelagia Philbert ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma baada ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake na miaka 40 ya Utumishi ikiendelea
Baadhi ya watoto wa familia ya Mwl. Pelagia Philbert wakiendelea na Ibada


Baadhi ya waalikwa wakishiriki Ibada hiyo iliyofanyika Nyumbani kwa Familia ya Mwl.Philbert F. Byabato Kijijini Kashambya -Gera mwanzoni Jumatatu ya Pasaka March 28,2016.
Ibada maalum ikiendelea.
Ni shughuli iliyoandaliwa vyema kwa mpangio mzuri na kuwahusisha watu kutoka maeneo mbalimbali

Taswira kibandani wakati Ibada Ikiendelea


Mara ya baada ya Ibada inafuata ratiba ya Waalikwa kupata chakula na Vinywaji
Baadhi ya wanafunzi waliopita mikononi mwa Mwl. Pelagia Philbert

Neno la shukrani kutoka kwa Mwl. Pelagia Philbert pichani ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma baada ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake na miaka 40 ya Utumishi.
Sehemu ya Waalikwa wakimsikiliza kwa makini mstaafu Mwl. Pelagia Philbert
Taswira eneo la meza kuu wakisikiliza neno la mstaafu Mwl. Pelagia Philbert
Ndugu Mwijage pichani ambaye ni mwenyekiti wa harakati za Ruzinga Day

Mwijilist akitoa Somo

Mdau Paul Rwechungura pichani kushoto ambaye ni rafiki wa familia akisalimia na Mwl.Philbert F. Byabato mwenyeji wa familia hii

Mlangira Fucas Lutinwa mmoja wa wanafunzi wa Mwl. Pelagia Philbert akimpongeza mwalimu wake

Mlangira Focas Lutinwa mara baada ya kumpongeza mwalimu wake.


Mh. Diwani wa Kata Gera Mwl. Henery Gabriel Bitegeko akitoa neno kwa niaba ya familia

Mwl. Pelagia Philbert anatumia fursa hii kutoa Utambulisho wa familia yake, watoto wake na wengine aliobahatika kuwalea .
Katika picha ya pamoja na watoto wao, wengine wakiwa na waume zao huku baadhi wakiwa wameweza kuonozana na wake zao

Wanaonekana watoto wa Mwl. Pelagia Philbert katika nyuso zenye furaha
Wakati tukiendelea na Matukio ya Shughuli hii BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241

Utambulisho ukiendelea

Pichani ndiye Mtoto wa Kwanza wa kuzaliwa na mstaafu Mwl. Pelagia Philbert
Sherehe ikiendelea pichani baadhi ya waalikwa wakipata Vinjwaji
Furaha kwa watoto baada ya kupata kile wanachostahili pia

Watoto wa familia ya ya Mwl.Philbert F. Byabato wa Kijijini Gera na Mkewe Mwl. Pelagia Philbert wakiingia Ukumbini kwa Shangwe na nderemo


Burudani wakati watoto wa familia hii wakiinia Ukumbini
Tukio linalofuata ni watu wate kupata huduma ya Chakula
Anaonekana Mama yetu Mwl. Pelagia Philbert akiwa ameongozana na waalikwa kupata msosi
Baba mwenye nyumba Mwl.Philbert F.Byabato pichani kushoto akipata huduma ya Chakula

Utaratibu wa kupata Msosi safi kabisa ukiendelea
Anaonekana mwanafamilia akiwa katika hekaheka za kuhakikisha Waalikwa wanapata Chakula
Wageni waalikwa wakiendelea kupata huduma ya Chakula
Watoto wa familia ya Mwl.Philbert F. Byabato wakibadilishana mawazo
Tukiwa bado eneo maalum kwa ajili ya kupata huduma ya Chakula, Endelea kufuatilia matukio mengine yaliyojiri katika hafla hii ya kumpongeza Mwl. Pelagia Philbert ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma
Sehemu ya watoto wakifurahia hafla hii ya kumpongeza Mwl. Pelagia Philbert ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma

Kila mtu aliweza kushiriki kikamilifu na kupata kile kilicho stahili

Watoto wakishushia Kinywaji mara baada ya kupata Msosi


Ndivyo anavyo onekana Mama yetu mpendwa mstaafu Mwl. Pelagia Philbert

Fursa nyingine ya Utambulisho kwa kuzinatia makundi mbalimbali

Hawa ni baadhi ya Wanafunzi waliopata kufundishwa na Mama huyu mstaafu Mwl. Pelagia Philbert


Shangwe za hapa na pale kutoka kwa  mmoja wa wanafunzi wa Mwl. Pelagia Philbert

Shukrani kwa kuchagua Bukobawadau ,Matukio ya picha 200 zaidi yanapatikana katika Ukurasa wetu wa facebook, jiunge nasi kwa kugonga LINK HII >>BUKOBAWADAU MEDIA
Next Post Previous Post
Bukobawadau