Bukobawadau

MAELFU WAHUDHURUA MAZISHI YA BALOZI JOSEPH CLEMENCE RWEGASIRA HUKO KANYIGO !!

Ni msiba mkubwa, kwetu na kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera lakini kubwa zaidi kwa familia yake, kifo ni kifo ila hiki cha Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira (81)kimeacha gumzo!
Pichani wanaonekana wakiwa na nyuso za huzuni wanafamilia ya Marehemu Mzee Rwegasira.
Baadhi ya Wanafamilia ya Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira muda mchache kabla ya Ibada ya mazishi kuanza .
 Maelfu ya watu wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara, na baadaye waziri wa Kazi na mwisho Waziri wa mambo ya nchi za nje,na Mbunge wa Nkenge mpaka mwaka 2000 Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira (81)
 Shughuli ya Mazishi haya imefanyika Nyumbani Kijijini kwa Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira Kanyigo -Bukoba jioni ya Jumanne March 8,2015
Prof Anna Tibaijuka mbunge wa muleba kusini akisaini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Joseph Rwegasira
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akisaini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha mhasisi wa Jimbo hilo, aliyekuwa Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Marehemu Balozi  Mzee Joseph Rwegasira
 Katibu wa CCM mkoa wa kagera Mama Costansia Buhiye akitokwa na machozi kabla ya kusaini.
 Mama Costansia Buhiye Katibu wa CCM mkoa wa kagera wakati wa kusaini kitabu cha Maombolezo ya kifo aliyekuwa Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Joseph Rwegasira katika shughuli ya mazishi iliyofanyika Jana March 8,2016
Katika utaratibu wa kusaini kitabu cha Maombolezo katika msiba wa Balozi Mzee Joseph Rwegasira
 Katibu wa Vijana Mkoa wa Kgera Bw Didas Zimbihile akisaini kitabu cha maombolezo
Prof .Kilahama akisaini kitabu cha maombolezo Kifo cha Mzee wetu Balozi Joseph Rwegasira.
 Mwenyekiti wa Shughuli ya mazishi haya akibasilishana  na Bi Jovitha
 Muda mchache kabla ya kuanza kwa Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Mzee Rwegasira
Bwana Julius Rwegasira akiwa amebeba Msalaba wakati mwili wa Marehemu mzee wake unatolewa ndani kwa ajili ya misa maalum ya mazishi
 R.I.P Mzee wetu Joseph Clemence Rwegasira
 Watoto wa marehemu jamani poleni sana
Jeneza  lenye mwili wa Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira likitolewa ndani
 Ibada ya Mazishi ya Marehemu Balozi  Mzee Joseph Rwegasira ikiendelea

 Kiongozi wa Kwaya akiongoza nyimbo za mababio wakati wa Ibada ya Mazishi
 Kwa ufupi ni kwamba watu ni wengi kweli kweli kutoka pande mbalimbali za nje na ndani ya nchi
 Kutoka Kushoto  pichani ni Adv Protas Ishongoma, Mr Rahym Kabyemela ,Bwana Rama na Mkubwa Majid Kichwabuta
Wanaonekana wanafamilia mwanzo wa Ibada ya mazishi
Wanaonekana wanakwaya pichani
 Ibada ya Mazishi ikiendelea....
Padre akiendelea kutoa mahubiri katika Ibada ya maziko ya Marehemu Mzee Rwegasira
 Mlangira Mzee Rugahibula pichani kulia akiendelea kushiriki Ibada ya mazishi ya rafiki yake mpendwa Marehemu Balozi Mzee Joseph Rwegasira.
 Waumini wa Kikatoliki wakiendelea kushiriki Ibada ya Mazishi
Mama Hassan (Kushoto) na Mama K pichani kulia wakati Ibada ikiendelea
Tunamuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEEN!!
 Mapadre wakiendelea kuongoza Ibada hiyo iliyofanyika Nyumbani kwa marehemu Kanyio
 Nyimbo za mazishi ya kikatoliki zikiendelea na mapambio ya kumsifu Bwana
 Muonekano wa Jeneza lenye Mwili wa Mzee wetu Balozi Joseph Clemence Rwegasira
 Pichani kulia kabisa anaonekana mama Mjane wa Marehemu Mzee Joseph Clemence Rwegasira
 Watu ni wengi kama unavyoweza kujionea
 Timu nzima ya Bukobawadau tunatoa pole sana kwa ndugu wa familia na watoto wa Marehemu kuondokewa na mama mzazi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen!!
 Mratibu wa shughuli ya mazishi haya akitolea jambo ufafanuzi kulingana na ratiba
 Ndugu Japhet Rwegasira pichani kushoto
 Taswira mbalimbali Ibada ya mazishi ikiendelea
 Moja kwa moja kutoka kijijini Kanyigo kupitia Mtandao wako wa BUKOBAWADAU
Jeneza lenye mwili wa Marehemu likiwa limebebwa kuelekea eneo la makaburi
Anaonekana mwenye huzuni huku majonzi yakiwa yanamtoka Bi Jovitha
Mmoja kati ya waombolezaji akiwa na simanzi kubwa
 Sehemu ya tatu ya matukio ya picha 50 wakati wa  kutoa heshima za mwisho
 Wanafamilia wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Marehemu Mzee Joseph Rwegasira
 Hivi ndivyo Mzee wetu Balozi Joseph Rwegasira alivyo pumzishwa katika nyumba yake ya milele
 Sehemu ya wanafamilia wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kumuaga mpendwa wao


 Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Jaskon Msome akitoa heshima zake za mwisho
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera pichani ,Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Jaskon Msome akitoa heshima zake za mwisho
Kwa umuhimu wa kipekee kabisa Bukobawadau tunakufikishia tukio hili kwa Idadi nyingi ya picha.
 Baada ya matukio ya kutoa heshima za mwisho ifuatayo ni sehemu ya nne (4) eneo la Kaburi
  Waombolezaji wakiw na nyuso za huzuni wakati Mazishi yanaendelea.
 Makamanda wa CCM kutoka Missenyi wakiingiza Jeneza  lenye mwili wa Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira Kaburini
 Mwili wa Mzee wetu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira ukipumzishwa kaburini
 Taswira eneo la Kaburi, shughuli ya mazishi ikiendelea
 Adv. Protas Ishengoma, akishiriki mazishi ya rafiki yake mpendwa Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira
 Sehemu ya wanafamilia wakiweka Udongo kwenye kaburi la Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira
 Mzee Pius Ngeze akiweka udono kwenye kaburi la Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira
 Mjane wa Marehemu Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira pichani katikati
 Baadhi ya Watoto wa Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira wakiweka Udongo
 Kufikia hapa Bukobawadau Media tunatumia fursa hii kutoa pole kwa wanafamilia kwa ujumla.
 Kwa namna ya pekekee tunashuhudia msiba uliogusa hisia za watu wengi.
 Mjane wa marehemu na Watoto wa Marehemu Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa wao
 Mwendelezo wa matukio ya picha wakati wa kuweka mashada ya maua
  Mbunge wa Muleba kusini Prof .Anna Tibaijuka  akiweka shada la maua
 Utaratibu wa kuweka mashada ukiendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali
 Zoezi la kuweka mashada ya maua likiendelea
 Zoezi la kuweka mshada ya maua likiendelea
 BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka Shada la maua
 Mama Mdogo wa Marehemu Mzee akiweka shada la maua
 Muonekano wa mashada ya maua juu Kaburi la Balozi ,Mzee Joseph Rwegasira
 Mtoto akifurahia picha kama anavyo onekana akiwa amebebwa na Bi Joanitha Rwegasira
Mama Mjane wa Marehemu Mzee Joseph Rwegasira mara baada ya shughuli ya mazishi
 Taswira mbalimbali kutoka eneo la tukio
 Baadhi ya waombolezaji wenyeji wa Kanyigo pichani
 ENDELEA KUWA NASI KWA MTIRIRIKO WA PICHA  PICHA ZAIDI......
Kwa matukio zaidi ya picha za msiba huu na habari mbalimbali za Ulimweguni kote jiunge na Ukurasa wetu wa facebook kupia link HII BUKOBAWADAU MEDIA
Sehemu ya tano (5) Salaam za rambirambi
  Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge ameweza kuzigusa nafsi za watu wengi pale alipo mwelezea Marehemu Mzee Rwegasira kwa namna ya kipekee na mengine mengi aliyo yatendea Mkoa wetu wa Kagera na Taifa kwa ujumla
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kutoa salaam zake za rambirambi na ubani kutoka katika Ofisi ya Mbunge
Salaam za rambirambi kutoka kwa Katibu wa CCM mkoa wa kagera Mama Costansia Buhiye
 Salaam za rambirambi kutoka kwa familia ya Mzee Pius Ngeze
 Mchungaji wa Kanisa  la kiinjili la kiruthel KKKT  akitoa salaam za rambirambi
 Salaam za rambirambi kutoka kwa Mwakilishi wa Kanisa Jijini
 Mama Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba kusini akitoa salaam za rambirambi
Mwakilishi wa  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongela ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mh.Jaskon Msome akitoa salaam za rambirambi
 Mama Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba kusini akikabidhi  ubani kwa Mjane wa Marehemu mara baada ya kutoa Salaam za rambirambi
 Mama Barongo akikabidhi ubani wake kwa familia ya Marehemu mzee Rwegasira
 Utaratibu wa Kutoa salaam za rambirambi ukiendelea
 MWISHO BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
MWISHO KUPATA MATUKIO YA MAPOKEZI BONYEZA LINK HII KUWASILI KWA MWILI WA BALOZI JOSEPH RWEGASIRA MJINI BUKOBA
 Kwa matukio zaidi ya picha za msiba huu na habari mbalimbali za Ulimweguni kote jiunge na Ukurasa wetu wa facebook kupia link HII BUKOBAWADAU MEDIA

Next Post Previous Post
Bukobawadau