SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

08 April 2016

ASEMAVYO MDAU MWESIGA 'KAGERA YAGERA'

Kama kagera si wa mwisho kimaendeleo basi tuko katika nafasi ya pili kutoka mwisho. Inaumiza sana kuona mkoa uliokuwa namba moja ukishindana na KILIMANAJARO na MBEYA sasa hivi hata mikoa mipya imetutupa mbali. Kweli baadhi wana machungu ila pa kuanzia ni wapi? Je wapi kila mmoja wetu anaona gap ili liweze kuwekwa bayana? Je ni vema maoni na malalamiko yetu yakawa yanaishia kwenye blogs, or other online media? Je hamasa gani wewe na mimi tuweke? Je nini mrejesho au matokeo ya makongamanoo yaliyowahi kufanywa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mkoa wa kagera angalau kuona mpango wa muda mfupi. 
 Labda yapo kwa mnaoishi bukoba tujulishe jamani. ABAANA BASHOME, FRIENDS OF BUKOBA, KAGERA AGENT FOR CHANGE nk wapi mipango yenu. MAANA SIJUI HATA KAMA WABUNGE WA MKOA WETU HUWEZA KUKAA PAMOJA NA KUJADILI YAHUSUYO KAGERA.. MADIWANI JE KUHUSU HALMASHAURI ZENU? Ni mapema lakini mchuzi wa…………….. hunywewa ukiwa wa moto.
 Au ni sawa na theory za wanafalsa wa zamani G. Vico 16th -17th c na Ibn Khaldun 14-15th c waliotoa CYCLIC NATURE OF HISTORY. Kwamba lazima kuwepo upside and down kuwa hatuwezi kuwa juu siku zote? Lakini je mbona Kilimanjaro wapo juu. Mbona Mbeya wanakimbia. Je ni KAMUNOBELE?
Wenzetu wa Kigoma, Geita, Singida wana utashi wa maendeleo wanawaza kwa kina kusogea mbele, mfano baraza la madiwani kigoma ujiji wna mipango mizuri sana yakimaendeleo katika sekta zote. Hyo ni ujiji tu ukijumlisha wengne wanasonga.
Wasafiri mnaona singda wanavyo come up jaman, Dodoma mbali na kuwa makao makuu ya nchi ndo usiseme. Jamani hata Tabora, Shinyanga tu mji unauzidi wa Bukoba? Achana na miji ya mikoa jaman miji ya wilaya nayo inakimbizana inatuacha mfano mzuri ni KAHAMA mtu apinge kama Kahama si zaidi ya Bukoba. Waangalie WAKURYA

Chei shana bakaturoga anga tukeroga si? Are we thinking? Viongozi mko wapi? Najua hatuwezi kuwapima kwa miez michache lkn tupe matumaini ya short term plan huku tukiandaa kwa pamoja ;long term plan. Jamii ikishirikishwa na ikawa na utashi wa kweli tutatoka tulipo. Eilanga elayabayo zamani mwaa kowakubigamba mbakusheka busha.
Je ni baadhi yetu kutokuwa na mapenzi mema na kwetu maana nshakutana na wengi huwambii kitu kuhusu nyumbani anakwambia mi kwetu Mwanza or Dar es Salaam yaan aibu tupu.
Naomba nikomee hapo ni maumivu.

 CREDIT:Mwesiga Mwesiga

2 comment:

Anonymous said...

Mbona husema chochote kuhusu ujenzi wa chini ya ya vuwango wa daraja la Kanoni ambazo ni mango la kuingia Bukoba mjini. Hata katika enzi za mkoloni daraja hilo nilikuwa pana zaidi ya sasa. Ukiweza tafuta hituba ya Mhe. Salim Ahmed Salim aliyoitoa Bukoba wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani. Mbali na uongozi wa ngazi ZOTE kuchangia kuiteketeza Kagera, wanakagera nao wanahatia maana ndiyo chanzo chuo yote. Yalianza zamani na yamechukua muda mrefu. Kuyarekebisha kutachukua muda mrefu pia. Lakini inabidi kuwa mipango ya muda fupi na mrefu, tubadili tabia, tuwe wakweli, tuwe na moyo na uvumilivu tuoate viongozi waaminifu na wenye kuona mbali.

Anonymous said...

Mbona hukusema chochote kuhusu ujenzi wa chini ya ya viwango wa daraja la Kanoni ambalo ni lango la kuingia Bukoba mjini. Au ilikuwa "bado"? Hata katika enzi za mkoloni daraja hilo lilikuwa pana zaidi ya sasa. Ukiweza tafuta hotuba ya Mhe. Salim Ahmed Salim aliyoitoa Bukoba wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani. Mbali na uongozi wa ngazi ZOTE kuchangia kuiteketeza Kagera, wanakagera nao wanahatia maana ndiyo chanzo cha yote. Yalianza zamani na yamechukua muda mrefu. Kuyarekebisha kutachukua muda mrefu pia. Lakini inabidi kuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu, tubadili tabia, tuwe wakweli, tuwe na moyo na uvumilivu tupate viongozi waaminifu na wenye kuona mbali.

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU