SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

08 April 2016

KUHUSU MSANII WA MAREKANI 'KOKUGONZA'

You are right,Bukobawadau Kokugonza ni Mtanzania, ni mtoto wa marehemu Longino(Longfellow) Mugarula wa Kiziba, Kashasha karibu kabisa na chuo cha ufundi kashasha. baba yake aliishi Marekani, mbali na kuwa msomi mbobezi (PhD holder) alikuwa pia mwanamuziki maarufu. Ameimba nyimbo nyingi sana kwa lugha mbalimbali na ameishi katika nchi mbalimbali km Finland, South Africa, canada n.k. Na kote huko aliiimba kwa lugha zote za wenyeji.

Kokugonza ni mjukuu wa Mzee Martin e Mugarula, huyu alikuwa mmoja wa wasomi wa mwanzo kabisa wa sheria mkoani kagera. Alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya awamu ya kwanza, alikuwa hakimu, ofisa wa polisi nk. Alifariki ghafla hospitali ya mkoa wa kagera mwaka 1988.

Kokugonza ana dada zake wengine wawili ambao Longfellow aliwazaa hukohuko Marekani, wanaitwa Ntangilege na Tibeshara Mugarula. Inapendeza baba yao aliwapa majina ya asili kutoka Bukoba.
Kila la kheri,
F. Mugarula.

 Shukrani kwake F.Mugarula kwa ufafanuzi wa ziada ikiwa ni baada ya post yetu ya Juma lililopita iliyosema ;Je ulijua kuwa dada aliyetokea kwenye episode mpya ya Empire ni Mtanzania?! Anaitwa Koku Gonza, anakaa Chicago. Ni mwimbaji na anapiga piano na gitaa pia... Katika Empire anaonekana anamfundisha @yazzthegreatest kucheza piano
Shoutout to @kokugonza I see you doin big things!! I'm proud #Repost from @wakazimusic @Bukobawadu Media

2 comment:

Anonymous said...

Ahsante sana F. Mugarula. Vile vile Longfellow alikuwa mtu wa kwanza kutia nyimbo zetu za Buhaya katika record. Long Playing record (LP) yake inaitwa "KWETU" aliitoa 1972.

Tibeshara Mugarula said...

Wow she is my sister so excited to see her in this article so cool !

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU