Bukobawadau

MAANA YA BAADHI YA MANENO AMBAYO WANAWAKE HUTUMIA.

1. Sawa bwana (fine)
"Sawa" ni neno ambalo hutumiwa na wanawake kumaliza mabishano na mpenzi wake. Wakisema hivyo ujue wanahitaji mwanaume unyamaze hawataki kusikia mabishano na makwazo yako.
2. Dakika tano tu.
Kama mnatoka na yeye anavaa na akakwambia nipe dakika tano, wewe nenda sebuleni na washa television kunja nne na tizama video, maana dakika tano ni nusu saa kwa mwanamke. Dakika tano hua dakika tano kweli kama mwanamke akikwambia wewe ndani ya dakika tano uwe umerudi nyumbani.
3. Hamna kitu (Nothing)
Huu ni utulivu kabla ya kimbunga chenyewe. Hii inamaanisha kuna kitu na jiandae nacho. Mabishano yanayoanza na kukwambia hamna kitu huishia na neno "sawa" hapo juu.
4. Endelea tu na mambo yako (Go Ahead)
Hii inaanisha "jaribu uone" sio ruhusa ya kukuruhusu uendelee! Usiendelee kufanya hilo, acha kabisa. Akikubamba utawakumbuka washenga maana yatakuwa mengine! Unyumba utausikia ktk bomba, utavaliwa jeans na mzungu wa nne kila mlalapo.
5. Kushusha pumzi kwa nguvu (loud sigh)
Hiki ni kitendo lakini kina maana zaidi ya kitendo ni neno kabisa, ila kwa kitendo. Kushusha pumzi kwa nguvu inamaanisha kwamba anafikiria kwamba wewe ni mpumbavu na anashangaa kwanini anapoteza muda wake kusimama hapo na kubishana na wewe juu ya upumbavu uliofanya (nothing) (refer hapo nyuma namba tatu na usome maana ya nothing)
6. Hamna tatizo (that's okay)
Hii ni sentensi hatari sana kutoka kwa mwanamke akimwambia mpenzi wake. Humaanisha kwamba anataka kufikiri zaidi na zaidi kabla hajaamua kivipi na lini utalipa kwa makosa uliyofanya. Kama amekushtukia unamchepuko nje na akakwambia hivyo, mambo ya tendo la ndoa sahau! Itahitaji maarifa mengi kumrudisha katika truck!
7. Asante
Mwanamke akikwambia Asante wala usijiulize maswali mengi, wewe mwambie tu "karibu" ila kama akikwambia "Asante sana" na kuna kitu umemuudhi kamwe usimwambie "karibu", hapo hakushukuru kabisa, ukijibu hvyo ataona kweli ulidhamiria kutenda kosa ulilofanya.
8. Fanya utakalo (whatever)
Ni njia ya mwanamke kukwambia nenda zako, haunibabaishi (go to hell!!)
9. Usihofu kuhusu hilo, nimeshaelewa!
Ni mojawapo ya sentensi tata na hatari kutoka kwa mwanamke, maana ya hii ni kwamba mara kwa mara kuna kitu mwanamke amemwambia mwanaume wake akifanye ila hajakifanya. Hii baadae itapelekea mwanaume kumuuliza "kuna tatizo gani?" mwanamke jibu atakalompa ni atamwambia namba tatu hapo juu.
10. Kukiwa na maudhi ndani ya ndoa, tendo la ndoa kwa mwanamke ni karaha, hutamani hata kila mmoja alale chumba chake, hutamani kila siku umalize haja zako huko nje, ukirudi nyumbani ulale tu na usimsumbue.
Ni ukweli kwamba wanawake ni vigumu sana kuwaelewa , ila vyovyote vile jinsi walivyo, wanawake ni uumbaji bora kabisa wa Mungu alioufanya. Kuwa na mwanamke ndani ya nyumba ni pambo tosha la nyumba yako, mahala popote pale palipo na wanawake, wanaume hupata utulivu wa nafsi!
Keep Smiling .. Smile, It’s Sunnah!
Jumaa Kareem!
Share
Mwl Tweve Hezron
Next Post Previous Post
Bukobawadau