Siku moja professor wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi wake wajiandae na Test anayowapa muda huo huo.
Wanafunzi walisubiri kwa uoga mno hasa ukizingatia aliwaambia ghafla
mno. Professor aliwagawia karatasi za maswali huku upande wa maandishi
akiufunika chini na kuwatamkia kwamba yeyote asifunue karatasi mpaka
atakapowaruhusu.
Baada ya kumaliza kuwagawia karatasi ya maswali kwa wote, professor akawaambia wafunue karatasi na kuanza kufanya mtihani.
Kwa mshangao, kila mtu akaona ya kwamba hakuna maswali yoyote katika
ile karatasi, isipokuwa nukta kubwa nyeusi katikati ya karatasi.
Professor baada ya kuona mshangao kwa kila mwanafunzi, akawaambia hivi,
"nataka kila mtu aandike kuhusu anachokiaona kwenye karatasi"
Wanafunzi wakachanganyikiwa, na kuanza kuandika vitu ambavyo hawajazoea.
Baada ya muda kwisha, Professor alichukua karatasi zote na akaanza kusoma majibu ya kila mmoja mbele ya darasa.
Wanafunzi wote walikuwa wameelezea ile nukta kubwa nyeusi, wakaelezea
'position' yake katikati ya karatasi, rangi ya ile nukta n.k.
Baada ya professor kumaliza kusoma majibu ya wanafunzi wote, darasa lilikaa kimya na Professor akaanza kuelezea.
"Sitaenda kuwapa marks kwenye hii Test, nilitaka niwape tu kitu cha
kuwafikirisha. Hakuna hata mmoja aliyeandika na kuelezea kuhusu sehemu
nyeupe ya karatasi. Kila mmoja wenu amelenga kwenye nukta kubwa nyeusi
iliyokuwa katikati ya karatasi.
Hii inatokea katika maisha yetu
ya kila siku. Tunasehemu nyeupe ndani ya maisha ya kufurahia lakini
tumejikita katika nukta nyeusi. Maisha yetu ni zawadi tuliyopewa na
mwenyezi Mungu iliyojaa upendo na kujaliana, tuna kila sababu ya
kusheherekea asili hii inayojijenga kila leo. Marafiki tunaokutana kila
siku, shughuli zinazotuingizia kipato, familia zetu pamoja na ndugu.
Hata hivyo tumejikita katika kutizama nukta nyeusi, mambo ya afya
yanayotusumbua, kukosekana kwa pesa, mahusiano magumu, na kukatishwa
tamaa na marafiki, mambo yote haya ni nukta nyeusi katika maisha yetu
meupe.
Nukta nyeusi ni ndogo sana ukifananisha na kila kitu
ambacho tumejaliwa nacho na Mwenyezi Mungu. Ila ndicho kitu
kinachochafua akili zetu.
Ondoa macho na masikio kutoka nukta
nyeusi katika maisha yako. Furahia kila Baraka uliyopewa na mwenyezi
Mungu, furahia maisha na ishi maisha yaliyojaa Upendo."
Share
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment