Bukobawadau

UMUHIMU WA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO!

Kama mwanaume hakupigii simu au hata ujumbe mfupi wa maneno kukujulia hali ila wewe ndio wa kufanya hivyo kila siku ni kwa sababu hataki kukupigia simu wala kukutumia sms.
Kama hataki kukupa 'attention' na kudai yuko busy kila siku ni kwamba hataki kuonanana na wewe.
Kama ataku 'treat' kama takataka ni kwa sababu hakujali.
Mwanaume ambae umekuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu kidogo anapokuambia kuwa "subiri kwa sasa sipo tayari" kwa kifupi ni kwamba hakupendi.
Usiendelee kucheza mchezo wake uletao hasira, 'don't keep playing his confusing game', usimtafutie sababu za kuendelea kumuamini!
Ngoja nikuibie siri mwanaume anapotaka kuwa na mwanamke hudumu naye pasina uongo, sababu au 'complications' zozote!
Acha kuendelea kusubiri ahadi zake za sungura na fisi, anachukulia faida uwepo wako, afanye yake na mwisho wa siku anaolewa mwingine. Weka utu wako mbele, na thamini ndoto zako!
Hauhitaji mtu ambae hajui ni nini anakitaka, hauhitaji mtu ambae hajui thamani uliyonayo kama mwanamke.
Unahitaji mwanaume ambae anatambua thamani yako na anakupigania kila siku. Acha kuendelea kuumiza moyo wako kwa mtu ambae hayupo kama ulivyomtegemea.
Mwanaume ambae anamlaumu kila mtu katika mambo yake isipokuwa kujilaumu yeye mwenyewe hafai kama ukoma!
Tumbua jipu hilo....
Weekend Njema, na Mwenyezi Mungu awabariki.
Share
Tweve Hezron
Next Post Previous Post
Bukobawadau