Bukobawadau

ASKOFU DK. ABEDNEGO NKAMUHABWA KESHOMSHAHARA AZURU MIJI YA NEW YORK, CHICAGO & MINNEAPOLIS, MAREKANI

Bishop Keshomshahara preaching in New York
Askofu Dk. Abednego Keshomshahara, Bibi Melisa Keshomshahara na Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mchungaji Elmereck Kigembe watembelea Marekani mwezi  Mei 2016.  Mei 15 hadi 21 walikuwa New York ambapo walihudhuria mkutano mkuu wa Synod ya Metropolitan New York ya Kanisa la Kiinjili Kilutheri Marekani inayoongozwa na Askofu Robert Alan Limbo. 
 Bishop Keshomshahara with ELCA African National Leaders
 Bishops Limbo & Keshomshahara sign companionship contract in New York
 JOKUCO Foundation Meeting- Chicago
 Tumaini Swahili Chapel Chicago
 Mei 22 - 30 walikuwa Chicago na walipata fursa ya kukutana na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Marekani akiwemo Mkuu wa Kanisa hilo Askofu Elizabeth Eaton.  Mwisho kabla ya kuondoka walifika Minneapolis, Minnesota walipokutana na Watanzania & marafiki wa Tanzania.  Kwa ujumla ziara yao ilikuwa na mafanikio makubwa muno.

Next Post Previous Post
Bukobawadau