Bukobawadau

MESSI ATANGAZA KUSTAAFU TIMU YAKE YA TAIFA

 Mchezaji wa Argentina na Barcelona Lionell Messi akihudhunika baada ya kukosa penati
 Mshambuliaji nyota wa Argentina na Barcelona Lionell Messi amestaafu kutoka kwa ulingo wa kimataifa wa soka. Lionell aliyasema haya muda tu baada ya timu yake ya Argentina kupata kichapo kutoka kwa timu ya Chile.

Messi, 29, alionyeshwa kutooridhika kwake na matokeo hayo na kuwaambia wanahabari kuwa "nilijaribu kufanya vyema kwenye mechi hii lakini sikuweza kufaulu, inahuzunisha kuwa sikupata ushindi...Hii ni mara yangu ya mwisho kushiriki katika mchezo wa soka wa kitaifa''.
 Hivi ndivyo chile walivyotwaa kombe la Copa Amerika
Next Post Previous Post
Bukobawadau