Watu kadhaa wamefariki
dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyotokea wilaya ya Kilosa
ikihusisha basi la kampuni ya OTTA CLASSIC
yenye namba DGK T.201
lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea jijini Dar ambalo limegongana na
lori la mafuta lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.
Waliofariki dunia ni pamoja na madereva wawili na wasaidizi wao pamoja na abiria wengine.
Miili ya marehemu imekimbizwa na mingine bado inapelekwa hospitali
ya mkoa wa Morogoro kwa utambuzi na kwa itifaki ila mahututi wengine
wanapatiwa matibabu hapo hospitali ya ST JOSEPH inayomiliikiwa na Kanisa
la Roman Catholic.
Rai:Kama una ndugu unahisi au unafahamu alikuwa anasafiri basi fanya mawasiliano naye mapema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment