Bukobawadau

SIMULIZI LETU LEO JUMAPILI JULY 24,2016

Miaka kadhaa iliyopita, hii ilikuwa nyumba ya hadhi ya juu kabisa katika jamii iliyopo hapo. Mmiliki wake alikuwa ni tajiri mno ambae kila mtu angependa kwenda kwake kuomba msaada. Hilo gari lilikuwa kivutio kwa kila mtu katika hiyo jamii. Ilikuwa kama ndoto iliyokuwa kweli baada ya mmiliki kuongeza gari na hiyo nyumba kama vitu anavyovimiliki.
Lakini leo hii, mali zimezeeka na kwa hali ya kawaida ya asili hiyo nyumba itabomolewa na atakuja mtu mwingine mwenye udambwi dambwi wa kutosha akasimamisha mjengo wa maana. Na hilo gari litapelekwa kwa wanunua skrepa.
Mtu atakayeishi kwenye nyumba kama hiyo HIVI SASA, pasina kumkufuru mwenyezi Mungu tunaweza tukamuona huyo mtu yupo katika daraja la chini kabisa la maisha.
Ni nini maana yake?
"Nothing in life is worth fighting for" Nguo yako unayoipenda sana kwa mwingine anaona kama dekio tu nyumbani kwake, akiba yako yote iliyopo benki kwa mwingine hiyo pesa ni ya mchango katika hafla fulani, girlfriend wako/ boyfriend wako/ mchumba wako alikuwa ni x wa mwingine. Kila changudoa unaemuona maeneo ya starehe kuna kipindi alikuwa bikra.
Ni nini maana ya haya yote?
Maisha ni mafupi sana kujihisi kuwa wewe bi bora kuliko mwingine. Steve jobs amewahi kusema "we all naked to death" kwa kiswahili "binadamu wote tu uchi mbele ya kifo" hakuna kitu kitakachotuokoa na kifo. Nimekua nikiona watu wakijikweza kwa utajiri wao. Uzuri wao, elimu zao na umaarufu.
Hakuna kitu ambacho utafanikiwa kukipata ambacho hakuna binadamu mwenzako amewahi kukipata. Kuna kitu kimoja tu ambacho wewe binadamu unapaswa kujivunia nacho. Ambacho ni "MAISHA YA KUMPENDEZA MUNGU" hivyo basi kuwa mwema kwa binadamu wenzako, acha dharau na nyodo. Siku zote Tengeneza marafiki na si maadui.
Kumbuka watu unaowadharau hivi sasa wakati upo juu, kuna kipindi utaanguka na utatamani msaada wao na usiupate. Hivyo basi usiwasababishie matatizo watu wengine kwa maana siku moja watakuja kuwa tatizo kwako. Usiendeshwe na umiliki wako wa mali kwa maana siku moja isiyo na jina mali itatoweka au wewe ndio utatoweka.
Tushikamane, Dunia itakuwa mahala salama pa kuishi kama tutauishi upendo ambao umekuwa ukifundishwa na vitabu vyetu vya dini.
Ni ujumbe wangu wa leo na ninawapenda sana.

Like Share It
Next Post Previous Post
Bukobawadau