Bukobawadau

BALOZI DR.KAMALA AENDELEA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KWA KASI KUBWA NA VITENDO

Balozi Dr Diodorus Kamala,Mbunge wa Jimbo la Nkenge wa tatu kutoka kushoto pichani alipotembele eneo Kijiji cha Ishozi katika Kata ya  Bugandika Wilayani Missenyi,eneo linalo lalamikiwa na Wananchi kuwa limehingizwa katika hifadhi ya Maliasili kinyume na utaratibu.
 Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Vijiji vya Bugango na Ishozi -Bugandika wakimuonyesha Mh. Mbunge wao  Balozi Dr. Kamala eneo linalolalamikiwa na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo. 
Eneo la wazi linalotumiwa na wafugaji wa maeneo haya
Makazi ya mmoja wa wafungaji wa eneo hili
Mch. Mageke Paul ,Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bugandika akichunguza Ubora wa Generator lililokabidhiwa shuleni hapo na Mbunge wa Jimbo wa Nkenge Balozi Dr. Kamala ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi zake alizo zitoa kipindi cha uchaguzi
Balozi Dr. Kamala kwa siku ya Jana ameweza kukabidhi Generator kwenye sekondari ya Bugandika iliyopo Wilaya ya Missenyi na kusaidia maeneo mbalimbali Kata Jimboni lake
Balozi Dr. Kamala amehitimisha ziara yake nyenye lengo ya kuziona kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Jimboni humo hususani ya Maji katika Vijiji vya Igulugati,Rukurungo -Bugandika,na ile ya Kilimilile,Ruzinga, Kenyana,Bugango na Kakunyu.
Mh Balozi Kamala alitumia fursa hiyo kuongea na wananchi katika kata zote 20 zilizopo Jimboni kwenye Jimbo la Nkenge ili kujua changamoto mbalimbali
pia ameweza kuchangia vikundi mbalimbali vya Wajasiliamali na miradi ya kimaendelea kwa kuchangia fedha,madawati na katika sekta ya michezo amechangia kwa kutoa Jezi na mipira kwa timu mbalimbali ili ziweze kushiriki katika mashindano Jimboni Nkenge.
Katika ziara hiyo Balozi Dr.Kamala amebaini kuwapo kwa migogoro mingi ya ardhi kuliko maeneo mengine nchini na kuwataka wananchi kusubiri matokeo ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa.
Mh Balozi Kamala alitumia fursa hii kuwataka wananchi kufanya kazi kiwa bidii ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya 'HAPA KAZI TU'.
 Balozi Dr. Kamala amewata wananchi katika vijiji mbalimbali kutokuendekeza unywaji pombe uliokithiri hasa nyakati za kazi na ameaagiza Aliwaagiza madiwani wote na watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kupambana na umaskini uliokithiri kwa wananchi.
Aidha Mh Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala katika ziara hiyo ya pili Jimboni kwake ameendelea kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa kipindi cha miaka mitano, pia kwa kumchagua kwa kura nyingi Mh John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuwachagua madiwani wa chama cha mapinduzi.
Diwani wa Bugandika Moody Migeyo akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano wa Mbunge Balozi Dr. Kamala uliofanyika jana Alhamisi Aug 18 katika Kijiji cha Ishozi
Balozi Dr. Kamala akisalimiana na Viongozi wa Kata ya Kashenye-Kiziba Wilayani Missenyi ,pichani katikati ni Diwani wa Kata Kashenye(Omulangira)Adeodatus Rugaibula.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Bwana Projestus Tegemaisho pichani.


Balozi Dr. Kamala akiongea na Wavuvi
Next Post Previous Post
Bukobawadau