TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini
Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Bukoba mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Wilfred Lwakatare.
Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Bukoba mjini.
Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Bukoba mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE
a. Ujenzi wa soko kuu la Bukoba, soko la Kashai na Stendi kuu ya mabasi Bukoba
b. Mikopo ya vikundi vya kijasiriamali vya akina mama na vijana
c. Urasimishaji wa makazi
d. Bima za afya kwa wananchi angalau 5000
Mada hii itatumika zaidi na Wana Bukoba kutupa taarifa.
Baadhi ya Washiriki watakuwa:-
1. Mh. Mbunge Wilfred Lwakatare
2. Katibu Alex Xavery (Katibu)
3. Happiness Essau (Afisa habari Bukoba)
4. Chief Karumuna (Mayor wa Bukoba)
5. Jimmy Kalugendo (Naibu Mayor)
6. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Bukoba mjini.
CREDIT :JF
Karibuni...