Bukobawadau

ALICHOKIHOJI LWAKATARE BUNGENI JANA

Ndugu Wananchi na wadau wa Bukoba Mjini na Kagera; jana nimepata fursa ya kuuliza swali ambalo limetuumiza vichwa wengi kuhusiana na mkoa wetu kuwa kati ya mikoa mitano maskini Tanzania kwa 39% ikizingatiwa kuwa mkoa wa Kagera una historia ya kuwa mkoa tajiri pamoja na Mbeya na Dar es Salaam miaka ya 1960 mpaka tulipokumbwa na vita ya Kagera-Uganda ambayo mpaka leo serikali haijawapa wananchi fidia iliyotolewa na Serikali ya Uganda.
Lakini pia mkoa wetu ulikuwa na shirika la BCU(Bukoba Cooperative Union) ambalo liliweza hata kuikopesha serikali. Leo hii hata Chama cha Ushirika KCU kimesambaratika kwa sababu za kisiasa.
Lakini pia, inatuwia vigumu kiziamini takwimu hizi. Je ni baadhi ya wilaya zenye umaskini au ni Kagera nzima?
Je, serikali imetuwekaje katika Mpango wa Matokeo Makubwa (BRN) ili kurudisha hadhi ya mkoa wa Kagera?

Yafuatayo ni Majibu ya Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Kijachi.
-Vigezo vilivyotumika katika kubainisha umaskini ni uwezo wa kaya kukidhi mahitaji ya msingi; chakula, mavazi na malazi. Utafiti wa 2011/2012 mkoa wa kagera una kiwango cha 39% ya umaskini.
*Ifuatayo ni mipango ya serikali katika kuinua uchumi wa Kagera:*
1.Kuendeleza maeneo yenye fursa za uwekezaji na viwanda vidogo na vya kati.kwa kuboresha miundombinu.
3. Serikali inahamasisha wananchi kuzitumia fursa na rasilimali zilizopo ili za kuwapatia kipato.
4.Serikali inaboresha upatikanaji wa pembejeo na masoko ya mazao na uvuvi yanayozalishwa na wananchi.
5. serikali ina mpango wa kuendeleza viwanda vya nyama ili kuendeleza sekta ya ufugaji.
7. Serikali iko mbioni kufufua viwanda vya nguo. Haswa mkoa wa Kagera.
8. Serikali mwezi Disemba itaanza utekelezaji wa kujenga reli ya kati kwa kiwango cha geji kuelekea Mikoa ya Magharibi ikiwemo Kagera ili kufungua fursa za uchumi.

NITUMIE FURSA HII KUWAAMSHA WAZAWA WA KAGERA WALIOKO NDANI NA NJE YA NCHI, KURUDI NA TUIJENGE BUKOBA KWA PAMOJA.
"mkataa kwao, ni mtumwa."

Imetolewa na:
Mh Wilfred Lwakatare
Mb.Bukoba Mjini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau