Bukobawadau

FAMILIA YA AL- HAJI ABBAKARI GALIATANO WASHIRIKI NA WADAU KATIKA DUA YA PAMOJA!

Familia ya Al-haji Abbakari Galiatano kwa ukarimu na upendo waungana na jamaa na marafiki wa familia Nyumbani kwa Bwana Abdul Galiatano katika dua maalum ya familia hiyo ya kuwaombea na kuwatakia maghufira ndugu zao waliotangulia mbele ya haki na kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha ndugu Abdul Galiatano kuingia katika nyumba yake. 
 Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa juma lililopita na kufuatiwa na pongezi kutoka kwa Viongozi mbalimbali na mawaidha yakuwataka wanafamilia kuendeleza upendo na mshikamano baina yao.
 Mzee Al haji Abbakari Galiatano akiendelea kushiriki  dua hiyo
 Baadhi ya ndugu na marafiki wa familia walihudhuria shughuli ya dua hiyo iliyofanyika Mwishoni mwa juma Nyumbani kwa Bwana Abdul Galiatano mitaa ya Omukigusha Mjini Bukoba.
Aliyesimama pichani ni Al haji Sadick Galiatano wakati mawaidha yakiendelea kutolewa
Kutoka kushoto pichani ni Khalid Galiatano, Badru.S.Galiatano na Abdul Galiatano

 Bwana Majid Kichwabuta  pichani
 Mdau Optaty Henry (Katibu) mmoja ya walioweza kushiriki dua hiyo
Shughuli ya dua ikiendelea.

Bi Mwajabu Galiatano na Bi Murungi Kichwabuta wakiweka ubani
Sehemu ya wadau wa familia ya Al haji Abbakari Galiatano wakiendelea kushiriki dua hiyo
Aliyewahi kushika wadhifa wa mkuu wa Mkoa na kustaafu Bw. Mohammed Babu pichani akitoa nasaha na shukrani kwa familia 
Bw. Mohammed Babu akiendelea kutia neno la shukrani.
 Sheikh akitoa nasaha zake kwa wanafamilia
 Bwana Majid akionyeshwa kuguswa na maneno ya Sheikh
 Vivyo hivyo haji Sadick akinyanyuka kwa ajili ya kumtunza Sheikh.
Sheikh akipongezwa baada ya kutoa  mawaidha yakuwataka na kuwahimiza wanafamilia kuendeleza upendo na mshikamano baina yao.
Baadhi ya wadau pichani walioweza kupata furasa ya kushirika shughuli ya dua hiyo
 Mrs Abdul pichani kushoto na Mama Mkwe wake ,Bi Mdogo wa Al haji Abbakari Galiatano
 Sehemu ya wanawake waliohudhuria shughuli hiyo,
 Kutakabaliwa kwa dua kunaendana na Chakula
 Baadhi ya washiriki wa shughuli hii wakipata huduma ya Chakula
 Wadau wakiendelea kupata chakula
 Kwa pamoja wadau wakishiriki chakula  mara baada ya dua
 Matukio zaidi ya picha yanaendelea...
Next Post Previous Post
Bukobawadau