Bukobawadau

MBOWE NA MBATIA WAWAFARIJI WANABUKOBA WALIOATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia leo jumanne septemba 13, 2016 wamewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Bukoba. Pia waliambatana na Mbunge  wa Viti Maalum Bi.Savelina Mwijake na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Chadema.Mbunge wa Bukoba Mjini akiteta jambo na Wafabiashara mbalimbali walioathiriwa na Tetemeko hilo kubwa Hapa Bukoba na huku kilio chao kikubwa kikiwa ni malimbikizo ya madeni yao kwa serikali ambayo mpaka wanapata hasara kubwa na kwa ujio huu mbaya wa Tetemeko la Ardhi wakidai zaidi ya Milioni 600.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi  James Mbatia(kulia) wakimsikiliza kwa makini mfanyabiashara huyo.
Janga la Tetemeko la Ardhi limewaathiri sehemu kubwa wafanyabiashara
Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambae ni Mtaalamu wa Masuala ya Maafa na Mwenyekiti  wa Ukawa amewaunga mkono Wanabukoba leo akiambatana na Mwenyekiti mwenza Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe kwenye safari ya kuwatembelea wahanga. Katika Safari hiyo wametoa misaada ya dharura kwa wahanga ikiwemo chakula, sukari, fedha na n.k na kesho Jumatano wataendelea na safari hiyo kuwatembelea Wahanga hapa Mkoani  Kagera katika sehemu mbalimbali. Leo wametembelea sehemu ya Kibeta, Hamugembe, Kashozi, Nshambya katika shule ya Ihungo iliyoathiriwa zaidi na Tetemeko hilo kubwa la Ardhi na kuwafanya wanafunzi kusimamisha masomo yao kwa wiki mbili kwa kukosa sehemu ya kusomea/Madarasa na Mabweni.

Msafara kuelekea Kata ya Hamugembe

Pia walitembelea Kituo cha Watoto Yatima Hamugembe chenye watoto 36 ambacho kipo chini ya mwangalizi Bi. Saada ambacho kimepata matatizo kwa Nyumba zake kuanguka chini na kuwapa na kuwafariji 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe akisalimiana na Bi. Saada mwangalizi wa Watoto Yatima

Wakiteta na Wanakijiji wa Kibeta sehemu Mama anayotokea Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Muganyizi Lwakatare
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akipata Ndizi kwenye Soko la Nyakanyasi wakati wa kuwatembelea Wahanga wa Tetemeko la Ardhi Bukoba leo.


Sehemu ya Majengo katika Shule hiyo kwa sasa baada ya kutokea Tetemeko

Tetemeko likiwa limeharibu sana sehemu kubwa ya Kanisa katika Shule hiyo ya Ihungo iliyopo kilometa 8 kutoka Bukoba Mjini

Taswira ya sasa Wanafunzi wa Shule ya Ihungo wakijipanga kuondoka Majumbani mwao baada ya Tetemeko la jumamosi kuwaathiri kiasi kikubwa na kushinikizwa kufunga shule hiyo kwa wiki mbili kupisha kuangaliwa upya kwa Shule hiyo kutokana na kuathiriwa na tetemeko.


Wakiwa Kanisani ndani, Kanisa lililojengwa miaka mingi iliyopita

Akiwa Kanisani hapo alipata muda akafahamu Viongozi mbalimbali katika picha waliopitia katika kanisa Hilo linalotimiza miaka 125 hivi karibuni lililozinduliwa mwaka 1892 likiwa ni kanisa la kwanza likifahamika Kashozi Parish.


Mh. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia pia alitembelea Kanisa la KashoziKanisa la Kashozi kwenye Taswira ambalo pia limepata shida kwenye Tetemeko la Ardhi lililotokea hivi karibuni siku ya Jumamosi sept. 10, 2016.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alipata nafasi akapata picha na Mama mlezi kanisani hapo ambaye alitambulishwa kuwa ana umri mrefu
Next Post Previous Post
Bukobawadau