Bukobawadau

STARTIMES KUONYESHA MICHUANO YA ULAYA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018




Na Dotto Mwaibale

MATAIFA 54 ya Barani Ulaya siku ya Jumapili hii yatashuka dimbani katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu ili kuungana na mwenyeji nchi ya Urusi katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini humo mwaka 2018.

Akitoa taarifa hiyo ya kusisimua kwa mashabiki wa soka nchini Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif amesema kuwa hii ni habari njema kwa wateja wetu na watanzania kwani wataweza kufuatilia kwa ukaribu kabisa mechi zote moja kwa moja kwenye runinga zao.

“Michuano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwenye kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi mwaka 2018 kwa nchi za Ulaya itakuwa ni yenye ushindani mkubwa ukizingatia ubora wa timu na wachezaji wake. Kwenye michuano hii mashabiki wataweza kujionea moja kwa moja mabingwa watetezi Ujerumani watakapoanza safari yao ya kulitetea kombe hilo kwa kuvaana na Norway. 

Pia macho ya wapenzi wengi wa soka watapenda kuiona Uingereza ikiwa chini ya kocha wake mpya Sam Allardyce watakaposhuka dimbani kucheza na Slovakia.” Alisema Hanif

“StarTimes inayofuraha kuwataarifu watanzania kwamba mechi zote za michuano hii zitaonekana moja kwa moja kupitia chaneli zetu mahususi kabisa za michezo ambazo ni Sports Focus, Sport Arena, World Football, Sport Arena na Sport Premium. 

Tunafahamu ya kwamba soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nchini, na sisi tupo katika kuhakikisha kuwa hilo linawezekana kwa gharama nafuu kabisa.” Aliongezea Hanif

Mabingwa wa kombe la EURO mwaka 2016 timu ya Ureno nayo itashuka dimbani siku ya Jumatatu ya Septemba 5 kwenye mchezo wa kundi B dhidi ya Uswisi jijini Basel bila ya nahodha wake Christiano Ronaldo ambaye bado anauguza jeraha la goti ambalo lilimfanya atolewe kwenye kipindi cha kwanza kwenye fainali za EURO zilizofanyika nchini Ufaransa.

“Michezo na burudani ni maudhui ambayo tunayatilia sana maanani StarTimes na ndiyo maana kila kukicha tunazidi kuongeza zaidi. Wateja wetu kwa malipo ya gharama nafuu kabisa ya mwezi wataweza kutazama mechi zote za michuano hii moja kwa moja kwenye chaneli tano tulizonazo mahususi kwa michezo pekee. 

Ninawaomba watanzania kuichangamkia hii fursa kwa kujiunga nasi na kufurahia kwa pamoja mchezo wa soka kupitia visimbuzi vyetu.” Alihitimisha Hanif

Ratiba ya michezo itakayopigwa siku ya Jumapili ya Septemba 4 ni: San Marino na Azerbaijan (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Focus), Slovakia na Uingereza (saa 1:00 usiku chaneli ya World Football), Lituania na Slovenia (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Life), Denmark na Armenia (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Arena), Kazakhstan na Poland (saa 1:00 usiku chaneli ya Sports Premium), Romania na Montenegro (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Life), Jamuhuri ya Czech na Northen Ireland (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Premium), Norway na Ujerumani (saa 3:45 usiku chaneli ya World Football) na Malta na Scotland (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Arena).

Michezo ya siku za Jumatatu ya Septemba 5 ni: Georgia na Austria (saa 1:00 usiku chaneli ya World Football), Croatia na Uturuki (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Life), Ukraine na Iceland (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Focus), Wales na Moldova (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Premium), Hispania na Liechtenstein (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Arena), na Israeli na Italia (saa 3:45 usiku chaneli ya World Football).

Na michezo ya siku ya Jumanne ya Septemba 6 ni: Uswizi na Ureno (saa 3:45 usiku chaneli ya World Football), Bulgaria na Luxembourg (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Focus), Sweden na Uholanzi (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Premium), Belarus na Ufaransa (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Arena), na Cyprus na Ubelgiji (saa 3:45 usiku chaneli ya Sports Life).

Michuao hii ya kuwania kufuzu kwenye kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 inaundwa na makundi tisa ambayo ni:

Kundi A ni: Netherlands, France, Sweden, Bulgaria, Belarus na Luxembourg; Kundi B ni: Portugal, Switzerland, Hungary, Faroe Islands, Latvia, na Andorra; Kundi C ni: Germany, Czech Republic, Northern Ireland, Norway, Azerbaijan, na San Marino; Kundi D ni: Wales, Austria, Serbia, Republic of Ireland, Moldova, na Georgia; Kundi E: ni Romania, Denmark, Poland, Montenegro, Armenia, na Kazakhstan; Kundi F ni: England, Slovakia, Scotland, Slovenia, Lithuania, na Malta; Kundi G ni: Spain, Italy, Albania, Israel, FYR Macedonia, na Liechtenstein; Kundi H ni: Belgium, Gibraltar, Bosnia and Herzegovina, Greece, Estonia, na Cyprus; Kundi I ni: Croatia, Kosovo, Iceland, Ukraine, Turkey na Finland.

Next Post Previous Post
Bukobawadau