Bukobawadau

ANAANDIKA ASKOFU KILAINI:Bukoba baada ya Tetemeko

Bukoba baada ya Tetemeko
Leo nilikuwa katika parokia ya Kashozi ambayo ndiyo parokia ya kwanza katika mkoa wa Kagera ilifunguliwa mwaka 1892. Kanisa lake lilijengwa mwaka 1902 na kumalizika mwaka 1907. Katika tetemeko hili lilipata nyufa nyingi na kuta zake nyingine zikapinda na kuwa hatarishi. Sasa waamini wanasalia nje. Tunawashukuru maaskofu waliotusaidia, sasa tumeweza kuwajegea banda kubwa la kusalia kama mnayoliona katika picha hii. Bado kuna changamoto kwa mfano mvua ilinyesha kidogo wakati wa kipaimara na watu wakavumilia tu.. Mapadre bado hawana mahali pa kuishi wako katika namna ya dormitori ambayo hata hivyo nayo ina nyufa lakini hawawezi kuacha kondoo wa Bwana. Lakini bado kuna parokia nyingine ambazo hata msaada huu haujafika. Watu kila mmoja ameguswa hivyo hawana uwezo wa kuchangia lakini wana imani kubwa na wanasalia nje. Tunamshukuru kila mmoja anayetusaidia katika hili. MUNGU NI MWEMA KILA WAKATI
Kashozi is the first parish in Kagera region founded in 1892. Its historical church that preserved cardinal Rugambwa’s body for 15 year was hit by the earthquake and cannot be used. It has dangerous cracks and the walls are bent. Thanks to bishops of Tanzania’s help we were able to build them a large shed for Sunday mass. The priests are still sleeping in a damaged room but are steadfast together with their faithful. Many of the faithful had their houses damaged. We are grateful for any help we receive. There are other parishes that do not as yet have this basic assitance. 
GOD IS GOOD ALL THE TIME
Next Post Previous Post
Bukobawadau