Bukobawadau

MOTO ULIOIBUKA ENEO LA KIJIJI KATARABUKA BWANJAI NA KUZUA TAHARUKI SIO VOLCANO !

 Kumekuwa na taarifa za kuzuka kwa  milipuko  ya miale ya moto eneo la  Kashalu(karibu na shule ya msingi Katarabuga)iliyopo Kata Bwanjai- Tarafa ya Kiziba(Wilaya ya Misenyi) Jioni ya leo ,hali iliyozua taharuki kwa wananchi wakidhani ni Volcano kabla ya wataalam kufika eneo la tukio na kudhibitisha kuwa kilichotokea sio Volcano.
Kutoka eneo la tukio pichani kulia ni Mku wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denis Mwila akitolea jambo ufafanuzi,Missenyi Luteni Kanali Denis Mwila ameongozana na mtaalam Prof Mluma Abdulkarim ambaye ni Mtendaji mkuu wa wakala wa Geologia nchini alidhibitisha kamba kilichotokea ni tukio la kawaida sio Volcano.
 Kilichotokea ni maozo ya Vitu kama mbolea, magome ya miti na nyasi kupata moto unao onekana kufuka juu ya ardhi ingwa kwa siku ya kesho uchunguzi zaidi utafanyika ili kujua ni nini asa kilichotokea katika eneo hili la Katarabuka Bwanjai Wilayani Missenyi
 Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala pichani kulia aliweza kufika eneo la tukio mara baada ya taarifa hizo kumfikia akiwa katika ziara Jimboni mwake

Mashuhuda wakiendelea kufuatilia kilichotokea na kuzua hali ya taharuki 

 Kama unavyojionea pichani Kilichotokea wala hakishabihiani na i volkano kwani ,volkano inaambatana na mlipuko mkubwa wenye tope la moto litokanalo na miamba iliyoyeyuka na kubadilika kuwa tope (magma) Tope hili huruka juu sana na likirirudi chini huanza kutiririka kwa kilometa kadhaa kama mafuriko. Kila tiririko linapopita hilo tope na kupoa hubadilika na kuwa mwamba mpya (lava) juu ya ardhi na mahali pengine huwa ni udongo unaojulikana kama volcanic soil ,Ardhi kama hiyo ipo Kilimanjaro.
#Bukobawadau Oct 6,2016
Next Post Previous Post
Bukobawadau