Bukobawadau

RC ARUSHA NUSRA WAZICHAPE NA MBUNGE LEMA KATIKA UZINDUZI WA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO

 Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,wa kiwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambeye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na mtoto duniani Edru Broun
 wananchi waliouthuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto  ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa  aendelee kutoa hutuba
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo  ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo  ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa  ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na  mbunge  Lema.

Kabla ya vurugu  hizo mkuu  wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti  swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity  Afrika ).

Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga  mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema  alipo simama na kupinga hotuba hiyo  hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .
“mkuu wa mkoa acha kupotosha uma ,mchungaji simamisha hutuba ya mkuu wa mkoa imejaa siasa anaongea uongo anaongea vitu asivyo vijua,sitakubali huu uongo uendee siwezi kubali hutuba iendelee kwani anaongea uongo ,akitaka atumie nguvu ya polisi siogopi kufa ila nataka ukweli ,na aondoe siasa aseme ukweli hili jamboni lamaendeleo ya wananchi na nikwaifada ya wananchi haswa mama na mtoto tena wale wasio jiweza kwaiyo naomba mkuu wa mkoa acha uwongo”alisikika Lema akisema kwa sauti kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa.

Jambo hilo liliwalazimu baadhi ya wageni wa alikwa wakiwemo wakinamama kumpigia magoti mbunge huyo alionekana akiwa na jazba kubwa huku akimsogelea mkuu huyo wa mkoa swala ambalo lingeweza kusabisha uvunjifu wa  amani .

Licha ya Vurugu hizo na kelele za wananchi walionekana nao kupinga hotuba hiyo ya mkuu wa mkoa,Mkuu wa mkoa wa Arusha aliendelea kuhutubia  akiwa anaeleza kuwa eneo hilo lilitolewa na marehemu Nyaga Mawala kwa serekali ili liendelezwe  kwa kujengwa hospitali na mama na mtoto kitendo ambacho kiliendeleza kelele za wananchi zikipinga hotuba hiyo wakidai mkuu wa mkoa anapotosha .
“hili jambo sio la siasa tusiingize siasa ,na kama kunamtu anampango wa kufanya siasa apa anapoteza muda wake mimi ni mkoa na ninafahamu historia ya eneo hili”alisema Gambo

Kwa upande wake mfadhili wa maradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya Festula Duniani Dkt.Edru Broun  alieza kusikitishwa na tukio lilijitokeza na kuwataka viongozi waweke pembeni siasa zao na tofauti zao na wamatangulize mungu ili kutimiza shabaha ya ujenzi wakituo hicho cha hospitali kitakachoweza kumsaidi mama na mtoto.
Alisema kuwa ujenzi wa hopitali hiyo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni sita  na kwa awamu ya kwanza kiasi cha shili bilioni tatu kitatumika kujenga hospitali hiyo fedha ambazo zitatolewa na wafadhili kutoka shirika la mama na mtoto (martenity Afrika).

Kwa upande wake mwenyekit wa Tasisi ya maendeleo ya jiji la Arusha (ARDF) Elifuraha Mtowe Alisema kuwa eneo la kujegwa hospitali hiyo lilitolewa na marehemu Nyaga Mawala nakwa ARDF kupitia ofisi ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini  ndipo taasisi yao ya ARDF ikamamua kutafuta mfadhili ndipo walipompata MartenityAfrika.

Alisema kuwa tangu wampate mfadhili waliingia mkataba na wakakubaliana hospitali iishe ndani ya mika mitano lakaini mfadhili mwenyewe aliwaakikishia kuwa hospitali hiyo itaisha mapema iwezeka kwani itakamilika ndani ya mwaka mmoja tu ili mama na mtoto aweze kupata huduma kwa araka zaidi.


Awali mbunge Lema aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa mkoa huyo alikuwa amegoma kuja kuzindua hospitali hiyo hadi pale mbunge huyo alipoamua kumpiga simu katibu mkuu kiongozi John Kijazi na kumwambia kuwa mkuu wamkoa kagoma kuja kuzindua  hospitali hiyo ndipo katibu mkuu alipoamua kupiga simu wizara ya tamisema ambapo ndio walimpigia simu mkuu wamkoa ili aweze kufika kwenye uzinduzi huo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau