Bukobawadau

ANAANDIKA HAPPY KATABAZI:MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU

MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU

Na Happiness Katabazi

MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo Hana Hekima".

Nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya Biblia Kuonyesha matendo ya kishetani yaliyotendwa Jana hadharani na Kiongozi wa Kanisa la Maombezi nchini lenye masikani yake Ubungo Kibangu Dar Es Salaam,Anthony Lusekelo yana baraka  za kitabu cha Mithali 20:1 Katika Biblia Kwani matendo Yale aliyoyatenda ambayo nimeyaanisha Katika ndani ya makala hii ya lithibitishwa mtumishi Huyo wa Mungu Hana Hekima. 

Jana 23/11/2016   nikitoka nyumbani kwetu saa 11 asubuhi   Sinza  C nakuelekea  University of Bagamoyo eneo la Kawe Beach Dar es Salaam  Ambapo chuo hicho kimepakana na Ofisi ya Redio Times kwaajili ya kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma.

Hatua chache kabla ya kufika chuoni hapo ni kama nyumba  Tatu kurudi  nyuma  kuna Ukumbi unaitwa Mtana Multipose Hall  na katikati kuna barabara ya vumbi inayotenganisha nyumba zilizopo upande wa kushoto na kulia .Ni barabara ndogo ambayo Dereva hawezi geuza Gari  hadi aende Mbele zaidi.

 Upande wa kulia wa ukumbi huo wa Mtana Multipose Hall kuna nyumba  ya ghorofa ambayo inalimdwa na walinzi wa makampuni ya Ulinzi  ambao walinzi Hao  ni Waaafrika na wanaishi pia raia wa kigeni .

Nyumba ina namba  KAW / MZN/ 1348  ambayo imebandikwa katika ukuta wa geti la nyumba hiyo na mabango ambayo yanayoonyesha nyumba hiyo inalindwa na kampuni ya ulinzi nyuma ya nyumba hiyo ni  Bahari ya Hindi .

Saa 12: 32 asubuhi nilipita Katika njia hiyo nikiwa nimepanda usafiri wa aina ya Bajaji kwaajili ya kwenda Chuoni kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma  nilipofika  katika eneo la nyumba hiyo yenye namba KAW /MZN / 1348 
inayotenganisha nyumba zilizojengwa  upande wa kulia na kushoto na Kabla ya kufika chuoni ambapo ni mwisho kabisa ya barabara hiyo nyembamba nilikuta Gari limesimama katikati ya barabara yenye namba za usajili  T126 DFN  huku watu kama nane  wakiwa wamesimama pembeni ya Gari Hilo huku wakimtazama mtu mmoja aliyekuwa akiongea kwa sauti ya juu nje ya geti ya  nyumba hiyo.

Mimi nilipofika karibu nione kuna nini na kwanini Gari limeziba njia na nani Kaziba njia Yule anayeongea kama kuna ugomvi ninani niliposogea Karibu nikabaini aliyekuwa anafoka ni Mchungaji Anthony Lusekelo  maarufu " Mzee wa Upako.

Nilishtuka nikamtaka Dereva anishushe Mara Moja licha safari yangu ilikuwa haijafika mwisho licha ni Hatua Chache kufika chuoni Kwangu ili niwahi kwenda kumsihi Mchungaji Lusekelo aondoke eneo lile Mara Moja Kwani yeye ni kiongozi wa Kiroho na Mtumishi wa Mungu haifahai , kujibizana na watu tena hadharani Kwani mwisho wa siku anayedhalilika ni yeye.

Nilimkaribia Mchungaji Lusekelo na kumshuhudia kwa macho yangu akiwa anatoa lugha za matusi na zisizofaa kwa wakazi wa nyumba Namba KAW / MZN/ 1348 huku akiwa amesimama nje ya geti la nyumba hiyo ambayo wanaishi pia Raia wa kigeni huku akisikika akisema wamezidi kumchokoza kwa kumuita yeye ni Mlevi.Nilihisi  kuchanganyikiwa kabisa maana sikuamini nilichokuwa nilikushuhudia.

Mzee wa Upako ni miongoni wa wapenzi wa makala zangu    na zaidi ya Mara Tatu alishanipigia simu kunipongeza kwa ujasiri wangu wa kuandika makala zenye Lengo la Kujenga nchi na Akawa anasema ananiombea kwa Mungu azidi kunilinda ili niendelee kuandika.

Namimi pia nimekuwa nikifuatilia   mahubiri yake kupitia Televisheni ya Chanel Ten , Mara kwa Mara ila sikuwahi kubahatika kuonana ana kwa ana na yeye hadi Jana saa 12 asubuhi nilipomuona akiwa Katika Hali ile ambayo siyo ya binadamu wa kawaida .

Ambapo nilimsabahi nikamwambia Mimi ni Muhumini wake na ni mwanafunzi wa Univeristy of Bagamoyo chuo ambacho kipo nyumba ya pili kutoka nyumbani kwake .

Licha  ukweli ni kwamba Mimi siyo muumini  wa Kanisa lake . Nililazimika  kuficha jina langu ili asinijue kwani ningemtajia jina langu tu lazima angenifahamu kuwa mimi ni Mwandishi wa habari ' Mkonoko ' ambaye amekuwa akiwasiliana namimi na kunipongeza kwa makala zangu kwasababu  angekosa amani kwasababu Angejua waandishi wamemuona.

Kwa mujibu wa wale watu Saba  niliyowakuta eneo la tukio saa 12 asubuhi walinieleza Mzee wa Upako asubuhi hiyo alikuwa anatoka alikokuwa atatokea ndiyo muda huo alikuwa akirudi nyumbani kwake ndipo aliposimamisha Gari lake Hilo Mbele ya geti ya nyumba ya jirani yake yenye Na.KAW/MZA 1348 ambapo ndani ya geti Hilo kuna walinzi alianza kujibizana na walinzi akidai wamekuwa wakimkebehi yeye hafai Kuwa Mchungaji kwasababu ni Mlevi kupita kiasi.

Nilimsii sana hadi saa Moja asubuhi ikanikuta eneo Hilo la tukio huku Mvua ikitunyeshea nikimwomba anisikilize  aache kutukana,kufoka Katika eneo la nyumba ya watu kwasababu yeye ni mtumishi wa Mungu anajidhalilisha ,na anavunja  Sheria za nchi Kwani kutoa lugha chafu ni kosa la jinai,na pia kuziba njia ili watu wasipite kwasababu eti anaugomvi na wale watu siyo ustaarabu na anavunja Haki za watu wengine za kwenda Kokote watakako .

Sasa yeye Mzee wa Upako kwa kitendo Chake kile kuegesha Gari katikati ya barabara ile nyembamba ni kuvunja Haki za watu wengine wanatumia usafiri wa Magari Katika barabara ile wasiende wanakotaka kwenda kwaajili yake na kweli alifanikiwa Kuzuia Magari  yasipite eneo Hilo kwa zaidi ya muda Kadhaa huku Mvua ikinyesha na wengine wakichelewa kwenda Katika shughuli zao kwa muda .

Baadae alinisikia huku akiwa ameloana maana Mvua ilionyeshea alikuwa akisikika akinuka Pombe  huku akiyumbayumba akafungua Gari lake akatoa Kikapu kilichokuwa kinachupa za Maji ya Kunywa ,kavaa viatu Vya wazi  na kashika miwani huku akiwa amekunja suruali.

Nikamsaidia Kubeba miwani na funguo wa Gari tukaelekea    nyumbani kwake ambapo ni jirani kabisa na eneo la tukio huku tukinyeshewa na Mvua tutafika nyumbani kwake saa Moja asubuhi tukafunguliwa  geti na vijana wake nikamuingiza hadi ndani ya geti la nyumba yake  na vijana wake wakanihoji nimetoka na baba Yao wapi asubuhi ile maana ndiyo baba Yao anarudi nyumbani muda ule tangu alivyoondoka Juzi (Jumanne) .

Nikawajibu nimetoka aye nyumba za Mbele alikuwa akigombana kwa maneno ndiyo nikamuondoa eneo la tukio nakumleta nyumbani kwake hapo kama msamalia Mwema.

Vijana wake wakatukaribisha  Mimi na baba Yao ( Mchungaji Lusekelo)  .Mzee wa Upako huku akiendekea kuongea kwa sauti ya juu akaingia ndani na kile kikapu na Mimi nikampa ile miwani niliyokuwa nimeishika ,akaingia nayo ndani Kisha akarudi ndani ya uwa wake   akaanza  Kuwaeleza vijana wake Kuwa yeye hata siku Moja hataki kudharauliwa,kuonewa  na atapambana  .

Wakati huo Mimi ule funguo wa Gari bado nilikuwa nimeishikilia kwaajili ya kutaka niwape wale vijana wake waende kukichukua lile Gari lilokuwa eneo la tukio walilete nyumbani wa Mzee wa Upako ili wananchi wengine waweze kutumia ile barabara.

Mzee wa Upako baada ya kumfikisha nyumbani wake aliniambia anaishukuru sana kwa kumfikisha nyumbani salama  na akaniambia ananiheshimu sana Mimi ni kama binti yake ila nimsamehe sana yeye anarudi eneo la tukio kwaajili ya kuendelea kupambana na wale majirani ambao ni Wazungu.

Nilimsii  sana Aiingie ndani akaoge,alale  kwanini yeye mwenyewe ndiyo ameniambia muda ule wa asubuhi ndiyo alikuwa akirudi nyumbani kwake akitokea katika matembezi yake ya jioni lakini akakakata akaanza Kuwaeleza vijana wake amedhihakiwa kwa kuambiwa yeye hafai Kuwa mtumishi wa Mungu Kwani ni Mlevi sana wakati mtumishi wa Mungu hapaswi Kuwa Mlevi na kufanya vurugu.

Vijana wake wale walivyokosa akili na busara wakaungana na uamuzi mbovu wa baba ya I wa kurudi eneo la tukio wakati Mvua ikinyesha kwaajili ya kwenda kuendelea Kujibu mapigo. 

Kwa zaidi ya Mara Sita nikawabembeleza  wale vija na wake waache upumbavu huo Mzee wa Upako ni mtu mashughuli nchini na kiongozi wa kidini wasiruhusu tena baba Yao kurudi tena eneo la tukio kwenda tena kufanya Fujo siyo vizuri Kwani mwisho wa siku Atakayedhalilika ni baba Yao.

Nikawataka wale vijana wasikilize ushauri wangu wamfungie ndani Baba yao ( Mchungaji Lusekelo ) a kalale Kwani anaonekana amechoka sana hajapumzika maana kanieleza alfajiri ile ndiyo alikuwa akirudi nyumbani kwake.

Ili Mimi niwapatie ule ufunguo wa Gari la baba Yao ili wao vijana ndiyo waongozane na Mimi   nikawaonyeshe eneo la tukio na Gari lilipoegeshwa Katikati ya barabara ,wale vijana walinijibu ' uwa hawatakagi Ujinga'.

Haraka sana wakanitaka niwape funguo nikawapa , huku Mzee wa Upako  akiiondoka hapo ndani kwake kurudi Katika eneo la tukio Kujibu mapigo huku Mzee wa Upako akiwa miguu peku ,vile viatu vyake Vya wazi ( Open Shoes ) vyenye rangi nyeusi Nikiwa nimevishika Mimi wakitembea Mwendo haraka na vijana wake ambapo njia nzima Mzee wa Upako alikuwa akifoka na matope miguuni.

Na alipofika tena eneo la tukio la wale vijana wake huku Mimi Nikiwa nimebeba Open Shoes zake ambazo nimezipiga picha .

Tayari kulikuwa kumeishapambazuka watu wamejaa anaendelea kufoka Magari hawawezi kupita kwasababu Mchungaji Lusekelo aligoma kuondoa Gari lake katikati ya barabara huku akisema aondoi  Hilo Gari hadi Rais John Magufuli na RPC Simon Sirro waje ndiyo wataliondoa Hilo Gari.

Nilisikitika sana Kwani jitihada zangu za Kuzuia Mchungaji Lusekelo asidhalilike  Mbele ya umati wa watu kadri kunavyozidi  kupambazuka Kwani watu walizidi kujaa na kumshuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya huku akilindwa na vijana wake ambavyo Mtumishi wa Mungu hapaswi kuvifanya.

Nikahamua kukaa Mbali kujifanya natuma SMS Katika simu yangu Kumbe napiga  picha vile viatu vyake alivyoniachia ,na Gari yake iliyokuwa imageshwa katikati ya barabara Mbele ya geti la nyumba Na.KAW/MZA 1348 ambapo tukio Hilo la aina yake lilitokea hadi saa mbili asubuhi Jana .

Hata Hivyo wale wale vijana wake alinishitukia  napiga picha tukio lile walitaka kunipiga kisa nampiga picha baba Yao .

Kwa makusudi  Niliamua kukanusha Kuwa sijapiga picha na kusingizia Mimi Nina matatizo ya macho hivyo nilikuwa Nasoma SMS lazima simu niinue juu na nisogeze  karibu na macho yangu.

Mmoja wa kijana wake akanitishia kunipiga ikabidi nimbadilikie  na kumtaka kwanza anikome, cha pili jeuri ya kunipiga Hana,Tatu sikumtuma baba yake arudi alfajiri aanze kufanya vituko vile vya kujidhalilisha,nne nikamwambia yule kijana ni shetani mwenye Mkia  ndiyo maana wameshindwa Kumfungia ndani  Mzee wao ( Mchungaji Lusekelo ) aache kufanya Fujo Mbele ya umati wa watu wakati wana nguvu za kumzuia na baba Yao Huyo ni kiongozi wa kiroho anajishushia heshima.Akawa mpole.

Akageuka pembeni nikawaweka mkono wangu nyuma kiaina ,nikairusha  simu yangu kwa nyuma Kwenye  majani na kulikuwa na majani yanaunyevu unyevu wa Maji ya Mvua   ili hata akianza kunipiga na kunilazimisha nimpe simu ,ashindwe kuipata simu.

Kijana Yule ambaye alioneka ni mtu wa mazoezi na misuli alivyoona sijamuogopa Akaamua kuondoka nilipokuwa nimesimama mimi na akasogea  eneo la tukio na kumshuhudia Mzee wao  Mchungaji Lusekelo akizidi kufoka nikageuka nyuma haraka nikaokota simu yangu nikaenda kusogea Mbali nikampa mwanamke mmoja anayefanyakazi  chuoni kwetu anishikie tukasogea mbali na  aneo la tukio ,tukasimama  mbele ya geti la Redio Times na kuendelea   Kutizima  Sinema yote ilivyokuwa ikiendelea ambayo Mwongozaji wa Sinema alikuwa ni Mchungaji Lusekelo.

Kumbe vile vitendo vilivyokuwa vikifanywa na Mchungaji Lusekelo Jana Mbele ya Hadhara viliwakera   wakazi wa eneo hilo na watumiaji wa eneo hilo  licha ni la makazi ya watu lina Ofisi  pia na chuo wakaamua kupiga simu polisi kwa siri .

Baada ya muda mfupi polisi wa Kituo cha Kawe walifika eneo la tukio na kushuhudia tukio hilo na kuondoka na Mchungaji Lusekelo na kwenda kumuifadhi ndani ya kituo hicho kwa muda  kwa saa Kadhaa.

Hata hivyo taarifa toka ndani ya Kituo hicho zilieleza Kuwa licha ya Mchungaji Lusekelo kuifadhiwa ndani ya Kituo hicho  aliendelea kutoa lugha zisizo na staha kwa baadhi ya Askari Polisi ambao walikuwa wakimshangaa Kuwa imekuwaje yeye ni mtumishi wa Mungu halafu amekunywa Pombe kiasi kile na anatoa lugha zisizo na staha .

Hata hivyo mchana wa jana kuna taarifa ambazo hazikuwa  zimethibitishwa  Kuwa Mchungaji Lusekelo alihamishwa pale Kituo cha Polisi Kawe na kupelekwa Katika Kituo kingine.

Kwa mujibu maelezo hayo ya tukio Hilo la ' Sinema ya Bure' nililolishuhudia kwa macho yangu yaliyokuwa yanafanywa  na Mchungaji Lusekelo huku akiwa Katika Hali isiyokawaida kwa zaidi ya saa mbili ya kufoka na kutoa lugha chafu na kuleta Usumbufu Katika eneo la nyumba ya jirani yake  limenifundisha mambo mengi ikiwemo Mimi Leo kukubaliana ule usemi usemao ' Mungu adhihakiwi' Kwani ukimdhihaki atakuumbua hadharani.

 Mchungaji Lusekelo ni muhubiri maarufu nchini na ana waumini wengi sana nchini ndani na nje ya nchi na wamekuwa wakimuamini na hata serikali ya sasa inayoongozwa na Rais John Magufuli Inamuamimi na hata Rais Magufuli Mwenyewe siyo Siri anamuamini mtumishi huyu wa Mungu Mchungaji wa Lusekelo na alishampongeza Lusekelo kwa Kazi nzuri anayoifanya ya kutoa huduma ya Kiroho kwa Watanzania ambao ni waumini wake .

Juni 5 mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushitukiza katika kanisa hilo ambapo alienda kwaajili ya kusali katika kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo na Rais Magufuli akatumia fursa hiyo kuzungumza kanisani hapo eneo la Ubungo Kibangu na akamwagiza sifa Lusekelo Kuwa anafanyakazi nzuri ya Kiroho.

Magufuli akasema kwa  mamlaka aliyonayo ameishaagiza mamlaka zake zianze mchakato wa Kujenga barabara Inayopita Katika Kanisa la Mzee wa Upako ili waumini na wananchi wa eneo wasiendelee kupata tabu kwasababu barabara ile ni Mbaya sana.

Hata hivyo baadhi ya wananchi  walipinga uamuzi huo wa Rais Magufuli na walidai uamuzi huo ni wa upendeleo waziwazi na wakukurupuka.

Licha ya Lusekelo ya Kuwa na heshima kubwa nchini hadi Rais Magufuli Akaamua kwenda kusali kanisani kwake lakini Jana alishindwa kutunza Umaarufu wake,heshima yake aliyokuwa nayo Katika Jamii kama kiongozi wa Kanisa lenye waumini Wengi Akaamua kuporomosha matusi hadharani ,kuyumbayumba wakati amesimama Na kutembea Mithili ya mtu aliyelemewa na kilevi.  Uzuni.

Vituko vile alivyovifaya Jana Mchungaji Lusekelo pia vimenifundisha Mimi binafsi Kuwa kuanzia Jana niache tabia ya Kuwa mgumu kuamini /kunisha baadhi ya  taarifa za mambo  machafu yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wa Mungu.

Miezi mitatu iliyopita kuna watu watatu  toka vyombo Vya Ulinzi na Usalama walinieleza Huyo Mchungaji Lusekelo ni Mlevi mzuri tu wa Pombe aina ya Konyagi na wakati mwingine anavyokuwa madhabauni anavyokuwa na kitaulo anajifuta jasho mara kwa mara ni zile pombe kali zinakuwa zinachemka mwilini zinamfanya ajisikie jasho na walishamnasa katika matukio zaidi ya Mara Tatu  akiwa hoi kwa kilevi ,kwakeli nilikuwa mgumu kuwakubali maelezo hayo kwasababu kwanza sikuamini na niliwaona wale maofisa ni wazushi .

Ila Jana asubuhi nilichokiona kilichokuwa kikifanywa na Mzee wa Upako Mbele ya umati watu ,na alivyokuwa ananuka pombe ya kuyumbayumba nilikubaliana na Yale waliyonieleza watu wale na nikachukua simu nikamupigia mmoja baada ya mwingine na kuwaambia kweli waliyonieleza Leo Mungu amenileta eneo la tukio nithibitishe Yale waliyonieleza Kuwa Mzee wa Upako naye anakunywa Pombe.

Hata hivyo mama yangu Mzazi kwa zaidi ya Miaka mitatu  sasa tukikaa wote sebuleni tukiwa tunaangalia Kipindi cha Mchungaji Lusekelo kinachorushwa na Channel Ten ,mama amekuwa akiniambia huyu Mzee wa Upako ana michanganyo yaani alikuwa anamaanisha  Kuwa licha ni Mchungaji ila bado anafanya mambo ya kidunia ambayo Mungu hayapendi.

Basi mama akisema hivyo namwambia aache hiyo tabia ya kumsema Mzee wa Upako kwasababu Hana ushahidi.Mama anasema haya anafunga mdomo ila ipo siku Mungu atamuanika hadharani ndipo nitakapoamini.

Kweli kupitia tukio la Jana aliyofanya Mchungaji Lusekelo ,Nimelazimika kukubaliana na maneno ya Mama yangu Mzazi kuhusu Mzee wa Upako Kuwa licha ni mtumishi wa Mungu bado anafanya matendo ambayo Mungu hayataki 
 mfano Fujo, kutoa lugha zisizonastaa,kulipa kisasi wakati Mungu anatutaka tusamehe ,tusi lipe kisasi kwa watesi wetu lakini Mchungaji Lusekelo alishindwa kuwasamehe watesi wake na Akaamua Kupambana na maneno makali huku alipokuwa Kaipamba nao wakiwa wanamtazama hawamjibu.

Lusekelo ni binadamu kama Sisi ila tofauti yetu na yeye amejipambanua kama mtumishi wa Mungu ambaye ni kiongozi wa Kiroho hivyo Hakupaswa kufanya Yale yote aliyoyatenda Jana ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu ambayo kwa kiasi Fulani yalinivuruga  akili na akili zangu za kawaida Jana mchana.

Maana sikutengemea kumkuta kiongozi wa dini akiwa Katika Hali kama ile aliyokuwa nayo Mzee wa Upako na kufanya matendo Yale ambayo uwafanywa  na watu wasiyo na hofu na Mungu na hawajashiba  neno la Mungu.

Hata hivyo Fedhea iliyomkuta Jana Mchungaji Lusekelo pia naweza Kusema licha Mimi nilikuwa anajitahidi kumuokoa Lusekeo as izidi  Kuaibika Mbele ya watu Wengi Kumbe Mungu  naye aliamua kuruhusu mtumishi wake Huyo wa Mungu afedheheke  Mbele ya watu Wengi ili watu wa mjue Kuwa mtumishi Huyo wa Mungu ambaye Kutwa anahubiri   neno la Mungu naye Si Msafi  na kwamba anayefanya Mambo ambayo Mungu ameyakataza.Na kweli Mungu Jana kumdhalilisha kweupe Lusekelo. Mungu anatisha.

Nilikuwa najiuliza hivi ndiyo mmoja wa waumini wake angepata fursa ya kushuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya Mchungaji Lusekelo Jana au kama Alikuwepo muumini Akawa anashuhudia tukio lile ,wamejisikiaje? 

Hata hivyo tukio la Jana pia limenifanya nikubaliane na Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa madarakani alisema  hivi : ' Kuna baadhi ya viongozi wa dini Si wa safi,ni wachafu na wengine wanauza dawa za kulevya'.

 Nimuulize Mchungaji Lusekelo hivi kupitia tukio lile  ,atapata wapi tena ujasiri wa kusimama madhabau ni kuwataka waumini wake wasitumie vileo,wasilipize Ubaya kwa Ubaya ,wasiingie Katika vita ya maneno na watesi wao?

Sikutaka kuandika makala hii ila ni mejikuta nikijiuliza ni kwanini Mungu alipenda nikutane na Mchungaji Lusekelo kwa mara ya kwanza ana kwa ana akiwa katika hali ile na akiwa anafanya matendo yale ya kishetani?

Kwanini Mungu asingepanga nikutane na Mchungaji Lusekelo akiwa Mzima ananukia harufu  ya mafuta mazuri badala ya halufu ya kileo na akiwa anafokea na kutoa lugha chafu dhidi ya jirani yake na kuziba njia na kusababisha kuziba njia kwa muda na hali ya sintofahamu ?

Na Kwanini Mungu hakuruhusu waandishi wa habari wengine wapige asubuhi ile jana katika eneo hilo ili washuhudie tukio Lile isipokuwa mimi Mwandishi wa Habari Mimi Happiness Katabazi peke yangu?

Nikahitimisha  kwa Kusema Huyo  ni Mungu ndiyo aliyesababisha mimi nikutane na Mchungaji Lusekelo ambaye kwa zaidi ya miaka minne tumekuwa tukiwasiliana kwa simu ila jana nikakutana naye ana kwa ana na ndiyo  ananisukuma niandike makala hii ambayo imeanika   matendo hayo ya kishetani yaliyotendwa na Mchunga Kondoo wa Bwana  ( Lusekelo)  ili watu waumini wake na watu wengine wajue matendo yanayotendwa na Lusekelo  nje ya madhabau.

Na wao wenyewe wapi me Je  Mzee wa Upako ambaye ni kinara wakulusha ' Madongo' Je anastahili kuendelea kuaminiwa Kuwa kiongozi wa kidini na Baba wa Kiroho wa waumini wake ?

Nikajikuta nachukua Kompyuta na kuacha kwenda GYM kufanya mazoezi ya viungo  Jana jioni nikaa chini hadi saa Kumi alfajiri wa usiku wa kuamkia Leo nilipomaliza kuiandika.

 Kwa  kupitia makala hii ambayo itamfedhehesha Lusekelo kwa kiasi Fulani  na Imani kwa baadhi ya watumishi wa Mungu itazidi kutiliwa Shaka lakini neno la Mungu litasimama .

 Uenda makala hii  akiisoma anaweza kujirudi na asirudie tena Kutenda matendo yasiyompendeza  Mungu Kwani yeye Lusekelo ni mtumishi Mungu anapaswa asitende mat endo ya kishetani kama Yale  aliyoyafanya  badala yake abaki na kazi moja ya kumtumikia Mungu tu .Na ni aomba iwe hivyo.

Kwani hata EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Hivyo kupitia kitabu maneno hayo yaliyopo Katika kitabu cha Ezekiel ,Mimi nimeitimiza wajibu wangu kwako wewe Mtumishi wa Mungu Lusekelo kukuonea ili uache michanganyo ya mambo ya kidunia badala yake Ubaki na jambo Moja tu la kumtumikia Mungu.

Mchungaji Lusekelo Kumbuka  Biblia inasema Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu na hataki michanganyo.

Ukiamua kumtumaini / kumtumikia basi Ufuate mafundisho yake na uyatii  maandiko yake Kwani Mungu anauwezo wa kukuinua na kukushusha  pindi Akiamua.

Lusekelo Mungu ameinua huduma yako lakini sasa umeanza kurudi nyuma una michanganyo kama hiyo.Siyo vizuri .Mungu hapendi. 

Nina Hakika ungekuwa mzima usingetenda matendo ya kishetani uliyoyatenda Jana asubuhi Mbele ya kadamnasi .

Au ulivamiwa na mapepo ndiyo ya kakutuma  utende ushetani ule ambao ulikufedheesha ?Kwa lugha nyepesi ulikuwa umelewa .Aibu sana mtu wa Mungu.

Ingia ndani tubu kwa Mungu wako atakusamehe songa Mbele ila tu wale watu wote waliokushuhudia Jana ukiwa Katika Hali ile na kufanya vitendo vile Vya kishetani siyo rahisi tena kuiamini huduma ya Kimungu unayoitoa.Nisamehe sana.Licha Nitaendelea kukuheshimu na kukupenda.

Kama  kweli Mchungaji Lusekelo umeitwa na Mungu umtumikie ,sikutegemea kabisa mimi binafsi au umati ule watu huku ukiwa umelewa Pombe na huku hujavaa viatu   ukifanya ushetani ule hadharani tena asubuhi asubuhi. Inatisha.

Mchungaji Luseleko kama kweli umeweza Kutenda ushetani huo wa kuporomosha matusi hadharani ,nakuwa Katika Hali ile isiyoyakawaida ambayo unafahamu Mungu hataki matendo Yale ,Kesho wewe utashindwa kuingia tamaa ya kufanya mambo yasiyompendeza Mungu kama kwenda kufanya matendo ya kishirikina ili uwapumbaze waumini wako waendelee kuamini Kuwa ni mtumishi safi wa Mungu Kumbe unatenda matendo sirini yasiyompendeza Mungu?

Hivi Leo hii watu wakikurushia vijembe Kuwa Sadaka zinazotolewa na waumini wako pia unazitumia Katika ulevi ,Utakataa au utasema wanakuonea wivu?

Pombe inavishawishi Vingi sana na inaweza kumshawishi mtu aliyekunywa kufanya chochote anachokisia ikiwemo hata kufanya  zinaa.

Hivi ule ushetani ulioutonda Jana  wewe Mzee wa Upako ,wakiibuka watu wakisema unywagi Pombe tu pia hata dhambi ya uzinzi unatenda ,utakuja kukataa useme wakuzushie?

Pole waumini wa Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo Kwa makala hii Kwani nafahamu baadhi yenu itawakwaza ila ndiyo mvumilie ukweli ndiyo huo niliyoohushudia Mimi kwa macho yangu nanilitahidi kumsitili kiongozi wenu ili asidhalilike bila mafanikio na mwisho wa siku nilichoambulia nikutaka kupigwa na vijana wake .

Ila roho yangu nyeupe na wala makala hii haina Lengo la kuwazuia muache kumuabudu Mungu kupitia Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo.

Namimi ni madhaifu yangu sikatai ila bado sijafikia Hatua ya kama alifikia Lusekelo ya Kuwa mtumishi wa Mungu halafu kufanya matendo hayo ambayo kila Mara amekuwa akisimama madhabauni Kukataza waumini wake wasiyafanye kwasababu Mungu ameyakataza Kumbe yeye Anayafanya .

Lengo la Makala hii ni Kuonyesha Mchungaji Lusekelo ambaye anasimamaga madhabau ni anakemea dhambi Kumbe na yeye anatenda baadhi ya dhambi.Mtaamua wenyewe.Ila nawashauri sote tumuombee maana sote sisi ni binadamu Hakuna Mkamilifu .

Ila kuna utofauti wa upokewaji wa Jamii wa baadhi ya matendo ya dhambi yanayofanywa hadharani na viongozi wa kidini na matendo hayo hayo ya dhambi yakifanywa Na mtu ambaye siyo kiongozi wa kidini.

Mtumishi wa Mungu akitenda  dhambi za aina hizo alizozitenda Mzee wa Upako Jana za kutukana ,ulevi Jamii zitaipokea kwa uzito wa aina yake na kwa Mshangao mkubwa sana.

Hakuna ubishi Mchungaji Lusekelo umefedheheka Jana tena sana Katika eneo unaloishi Kawe Beach Karibu Univeristy of Bagamoyo na Redio Times .Kaa utulie,maana Hasira ya Mungu Jana imekushukia ,tubu Mungu atakusaidia uondokane na shetani wa Kupenda Konyagi na aina nyingine za Pombe Kali.

Mchungaji Lusekelo kama utashindwa kuachana na anasa za Dunia basi achana na Kazi ya Mungu ili uwe huru kufanya mambo ya anasa kuliko Jumapili na siku za katikati ya wiki Una Simama  madhabauni unaubiri neno la Mungu Kumbe ukitoka madhabauni unaenda kufanya mambo yasiyompendeza Mungu ukiwemo Kunywa Pombe.

Mchungaji Lusekelo jana kweli ilikuwa ni mara yako ya kwanza kunywa pombe kwa kiwango kile hadi zikakutuma kufanya matendo yale hadharani ambayo Mungu hapendi?

Je Mchungaji Lusekelo jana ni mara yako ya kwanza kurudi nyumbani kwako saa moja asubuhi ? Maana miminilikufika nyumbani kwako saa moja asubuhi huku nikiwa nimekubeba baadhi ya vitu vyako kama funguo wa gari ,miwani  huku wewe ukiwa umebeba Kikabu chenye chupa za maji ya kunywa ;

 Baada  ya kufanikiwa kumuondoa Kwenye eneo la tukio la ugomvi uliotokea na Kisha baada ya kukufikisha ndani ya nyumba yako wewe na vijana wako wewe ukatoka miguu pekupeku bila kuvaa viatu maana viatu ulikataa kuvaa nimevishika mkononi mkarudi tena eneo la tukio huku ukiwa Ujavaa viatu unakanyaga matope na Mvua inatunyeshea unafoka Katika nyumba ya jirani yako kuishinikiza walinzi wakifungulie Mlango uwaonyeshe Kazi?

Nakupenda kwasababu unapenda kuzungumza ukweli na mimi naupenda ukweli .

Hivyo nakushauri jirekebishe ,tubu kwa Mungu wako, na ukipata muda omba msamaha majirani zako kwa Usumbufu uliowasababishia Jana asubuhi wakuwazibia njia wenzio wasiende makazini na Magari Yao kwasababu Lako ulilipaki katikati ya barabara kumalizima tangu saa 12 asubuhi hadi saa mbili  huku ukisikia hutaliondoa Hilo Gari Hali RPC Sirro,Rais Magufuli waje kuliondoa. Nilikushuhudia ukiyasema haya sina Sababu ya kunisingizia .

Pia Hao vijana wako unaoishi nao hapo ndani baadhi yao wana akili mbovu wote watatu waliotufungulia geti kwasababu wao waliochangia kukurudisha tena   eneo la ugomvi Matokeo yake  ukaenda kudhalilika zaidi wakati Mimi nilifanikiwa kukuondoa  mapema eneo la tukio mapema na watu walikuwa  wachache na Magari yalikuwa hawajaanza kupita Wingi Katika njia ile .

Vijana Hao kama wangekubali ana na ushauri wangu niliyotoa wakati nome kufikisha ndani kwako wa kukuingiza ndani na kukufungia na Kisha wao vijana ndiyo ni wapeleke eneo la tukio niwape ufunguo wa Gari la Baba Yao Mchungaji wa Luseko wafike eneo la tukio wachukue Gari walioleta nyumbani bila kujibizana na watu kwani lakini walinipuuza Matokeo yake ndiyo hayo umati ulifurika ukakushuhudia ukibwatuka .

Polisi wa Kituo cha Kawe Dar es Salaam wakaitwa na wasamalia wema kwa siri wa kakukuta  eneo la tukio ukibwatuka  wakakupeleka kituoni ukiwa bado pombe hazijakuisha ukaifadhiwa  Kituo hapo kwa muda  ukasababisha hata Polisi ambao walikuwa hawafahamu Kuwa unakunywa Pombe wakajua,wakakudharau maana matendo yako ya Jana yalitukanisha pia watumishi wa Mungu .

Mchungaji Lusekelo na wale vijana wako mngeuzingatia ule ushauri wangu   Kuwa uende ndani ukaoge kisha ukalale  ile saa Moja asubuhi maana ulikuwa umechoka ungefanikiwa kukwepa Kadhia na Fedhea hiyo.

Mchungaji Lusekelo wewe ni mtumishi wa Mungu ,jiheshimu ,usijaribu kumgeuza Mungu Kuwa ni Mwanasesele labda aoni mambo unayoyafanya Gizani.Mungu siyo Mwanasesele anatuona yote tunayoyafanya hadharani na Gizani Akiamua kukuumbua anakuumbua na wewe Jana ni Mungu Yule ndiyo aliyekuumbua  hadharani kwakuonyesha wewe ni mtumishi wa Pombe, Haukulala nyumbani umerudi nyumbani kwako asubuhi, umeenda kufanya Fujo nyumbani kwa jirani na matusi ukayamwaga na ukawakera watumiaji wa barabara hiyo.Pole sana.

Na kukubaliana  na maneno haya yaliyoandikwa Katika  MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Na akosaye  kwa vitu hivyo Hana Hekima".

Kwasababu maneno hayo yametimia kwa Lusekelo ambaye alikuwa amepata kileo amefanya ugomvi na alipofanya ugomvi Jana alithibitisha umati ule wa watu  Hana Hekima Kwani Angekuwa na Hekima asingekubali kufanya ushetani ule  ambao umefedheesha Vya kutosha.

Naitimisha kwa kutoa ushauri wa viongozi wa dini akiwemo Mchungaji Lusekelo kama mmeamua kumtumikia Mungu basi mmtii Mungu kweli kweli Kwani sisi waumini wenu tunamuamini Mungu na Nyie viongozi wa dini sasa mnapokuwa mnafanya mambo ya kishetani Mnatupa wakati mgumu na kutuvuruga akili na kusabisha Kondoo mnaowachunga kutawanyika na wengine wanaamua kurudi kwa shetani. Mungu alishasema ole wake Mchunga Kondoo anayetawanya Kondoo wake .

Matendo kama hayo aliyoyafanya Mchungaji Lusekelo ndiyo yanayowatukanisha viongozi wa dini nakufanya wasiaminike Kumbe siyo viongozi wote hawana uadilifu wapo waadilifu na wameitwa kumtumikia Mungu na kuna viongozi ambao wao hawajaitwa kumtumikia Mungu na makanisa ni Biashara inayowaingizia picha .Mtalaaniwa na Mungu lazima.

Mungu Ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494.
24/11/2016.
Next Post Previous Post
Bukobawadau