Bukobawadau

KUHUSU AKAUNTI MBILI ZA MAAFA KAGERA

Na mwandishi wetu.
Bukoba.
KAMATI  ya maafa mkoani Kagera yatumia akaunti mbili kupokea fedha inayotolewa na Mashirika, Makampuni,tasisi na watu binafsi kwa ajiri ya kuchangia waathirka wa tetemeko la ardhi mkoani humo.

Kauli hiyo ilitolewa  Mwenyekiti wa kamati ya Maafa ambae ni mkuu wa mkoa huo Meja Jeneral mstaafu Salim Kijuu wakati akikabiziwa vyoo vya wanafunzi wa shule ya msingi Mgeza mseto iliyopo Manispaa ya Bukoba vilivyojengwa na shirika lisilo la kiserikali World Vision mkoa wa Kagera.

Kijuu alisema kuwa, akaunti hizo zinazopokea  na kutunza fedha za wathiriwa ni zile zinazotambuliwa na ofisi ya waziri mkuu ambazo ni akaunti maafa kagera na iliyopo kwenye ofisi ya waziri mkuu .

Alisema kuwa, fedha inayozungumzwa na kwananchi kuwa inatumika tofauti na malengo ya wachangiaji inatumika kulejesha  miundombinu mbalimbali sasa kwa ujenzi na ukarabati wa taasisi za umma shule zahanati barabara zilizokubwa na tetemeko hutolewa kwenye akaunti ya maafa kagera.

Aliongeza kuwa, kilichotumika kukarabati na kujenga ni shilingi bilioni moja, kilichobaki kwenye akaunti ni shilingi bilioni 4.2  ambachoo  kwa ukarabati wa shule za Ihungo na Nyakato inahitaji zaidi ya bilioni 40 ili kukamilisha na kuanza shughuli ya wananchi.

Aidha alisema wananchi wasikubakulinae na maneno ya kupotoshwa kutoka kwa wanasiasa kuwa makazi yao hayatalejeshwa na serikali kwa vile fedha inayochangishwa imetumika kwa ujenzi wa miundombinu inayohusu serikali.

"Mnachotakiwa kujua nikwamba serikali inampango wa kuwajengea makazi yenu kwa kuwapa vifaa vya ujenzi kwa kila kaya iliyopatwa na tetemeko hiyo wanasiasa wasiwapotoshe na kuona pesa imejenga miundombinu pekee." alisema Kijuu.

Hata hivyo alisema kuwa pesa iliyopo kwenye ofisi ya waziri ambayo ilifunguliwa kwa kupokea michango ya waathirika wanaochangia kutoka ndani na nje ya nchi haijatumika kwa kufanyia ujenzi wowote.

Aliongeza kuwa nyumba16000  za makazi ya wananchi zinazotakiwa kujengwa  zilizoanguka na zilizopata nyufa zitakarabatiwa  na  kujengwa kutokana na vifaa vitakavyotolewa kwa awamu inayofuata baada ya makundi maalum.

Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau