Bukobawadau

TAARIFA YA MRADI WA ''TUSHIRIKISHANE'' JIMBO LA BUUKOBA MJINI AUGUST-SEP, 2016

UTANGULIZI:Tushirikishane ni mradi unaowahusisha viongozi wa kuchaguliwa (mbunge na madiwani) serikali (halmashauri) na wananchi katika kufanikisha maendeleo. Wadau wakuu wa mradi huu ni Halmashauri ambayo ndiyo kitovu cha mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, Mbunge ambaye ni msimamizi wa serikali (halmashauri), Jamiiforums ambao ni wasimamizi wa mradi na Wananchi.

Tushirikishane ilianza rasmi mwezi August katika jimbo la Bukoba mjini kwa kukutanisha wadau husika. Kundi la wananchi liliwakilishwa na makundi yote wakiwemo viongozi wa dini, wanawake, vijana, wafanyakazi na wafanya biashara zote wakiwemo bodaboda, wazee n.k na kupitisha vipaumbele vinne ambavyo vimetokana na ahadi za mbunge alizotoa wakati wa kampeini. Vipaumbele hivyo ni;

1. Ujenzi wa Stand Kuu ya Mabasi, ujenzi wa Soko la Kuu na Soko la Kashai

2. Urasimishaji Makazi

3. Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na

4. Bima ya Afya
Utekelezaji wa mradi unaanzia Halmashauri ambayo inasimamia miradi yote na inayotokana na vipaumbele vyetu vinne (4). Pia inatoa taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vipaumbele vyote. Mbunge katika mradi ni daraja kati ya manispaa na wananchi katika kuweka msukumo wa utekelezaji na kutoa taarifa kwa wananchi. Mbunge pia anatoa taarifa kwa JF juu ya kila hatua zinazofikiwa katika vipaumbele vya mradi. Halmashauri na mbunge wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Jamiiforums ni mfatiliaji wa shughuli zote za mradi (utekelezaji wa vipaumbele) inatoa taarifa kwa wananchi juu ya mradi

Hatua zilizokua zimefikiwa katika vipaumbele vyetu mwezi August zilikua ni za kuridhisha isipokuwa mwezi September haukua wa mafanikio kabisa kutokana na athari ya tetemeko la ardhi. Kutokana na hilo ripoti hii itaanzia August ili kuweka mtiririko mzuri.
TAARIFA:
1.Ujenzi wa Soko Kuu
- Tayari vikao vya OGM (mhandisi mshauri) na CTM vimekwishafanyika kuhusu nyaraka mbali mbali kama feasibility study, architectural drawings, engeneering drawings, geotechnical survey, bills of quantities, na tender document

- Kampuni hiyo ya OGM imekwishawssilisha taarifa yake ya utendaji kuhusu utayarishaji wa nyaraka za mradi kwa kamati ya ilinzi na usalama

- Michoro ya jengo, usanifu na upembuzi yakinifu umekamilika ukionyesha basement, ground floor ghorofa tatu na tower
- Ukokotoaji wa gharama za ujenzi uko tayari umekamilika ambapo itagharimu shilingi 13 bilion

- Upimaji wa hali ya udongo tayari umekamilika

- Uchunguzi wa athari ya mradi kimazingira umekamilika

- Nyaraka za zabuni zimeandaliwa

- Mazungumzo kati ya OGM na TIB na halmashauri juu ya kupata pesa yamekwishakufanyika. TIB wameahidi kutoa 70% ya pesa yote na halmashauri kutoa 30% katika mapato yake au kwa ubia

- Baraza la madiwan limekwishakutoa kibali cha kukopa

- Akaunti maalum imekwishafunguliwa

- Aidha business plan haijakamilika kwasababu OGM waliomba kulipwa ghrama yao ya 50,000,000/- ili kukamilisha kazi hiyo lakin manispaa haikuweza kuipata kutokana na kushuka kwa mapato. Badala yake manispaa imeiandikia barua TIB kuomba kulipa kampuni ya OGM deni lake lote la zaidi ya mil 400 kama sehemu ya pesa ya mradi wa ujenzi wa soko kuu

- Maombi ya eneo la KCU lililoko kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa na Mkombozi Commercial Bank yalifanyika kwaajili ya kuhamishia wafanyabiashara wa soko kuu kwa muda ili kupisha ujenzi. KCU wamekubali kutoa eneo

- Hatua inauofuata ni kukaa uongozi wa halmashauri pamoja na uongozi wa soko na wafanyabiasha kuweka mikakati ya kusonga mbele, kutangaza na kupata mzabuni, kuhamisha wafanyabiashara, kutaguta pesa hiyo 30%, n.k
2. Ujenzi wa Stand ya Mabasi

- Fidia ya jumla ya 12, 967, 735/- imekwishalipwa kwa watu watatu ambao walikua hawajalipwa

- Eneo la hekta 6.53 limetengwa na kupimwa

- Mchoro umekwishaandaliwa

- Uchunguzi wa athari ya kimazingira umekwishafanyika

- Shirika la Mzinga Holding Cooperatio Ltd tawi la Morogoro limeingia makubaliano na manispaa lifanye kazi ya kuandaa feasibilitu study, ramani ya michoro na majengo, business plan, na kusaidia kutafuta mbia au mfadhili wa mradi

- Kazi zinazofuata ni kuandaa andiko la mradi na kutafuta fedha kwa wabia wau wafadhili ( Bank ya Dunia wameonyesha nia)
Pichani ni muonekano wa mazingira ya Soko kuu kwa hivi Sasa

3.Mradi wa Ujenzi Soko Kashai

- Michoro na usanifu tayari

- Andiko la mradi limekamilika

- Uchinguzi wa athari ya mrafi kimazingira umekamilika

- Nyaraka za zabuni zimekamilika

- Fedha za ujenzi bado zinaombwa kutoka bank ya dunia

4.Urasimishaji Makazi

- Zoezi la kuunganisha mitaa katika vikundi limekwishakamilika Kashai na Bakoba.

Kashai imewekwa katika vikundi vitatu;
i. Kashenya
     Kilimahewa
     National Housing

ii. Mafumbo
    Matopeni
    Lwome

iii. Kashai
    Kisindi
    Katatolwansi

Bakoba mitaa ni miwili;

i. Nyakanyasi
    Mtoni

ii. Forodhani
    Buyekela

- Gharama za kupima ni 200000 kwa kila nyimba ambazo zinawekwa katika akaunti za vikundi

- Tayari akaunti maalumu zimekwisha kufunguliwa kwa kata hizo mbili

- Wananchi wanaendelea kuelimishwa

Aidha, zoezi hili limeathiriwa sana na tetemeko la ardhi.

5.Mikopo kwa wanawake na Vijana.

- Halmashauri inatenga 10% ya mapato yake ya kila mwezi na kupeleka SACCOS kwaajili ya mikopo ya wanawake na vijana

- Uhamasishaji wa wanawake na vijana kujiunga katika vikundi unaendelea katika ngazi ya kata

- Elimu ya ujasiriamali inatolewa

- SACCOS mbili zitakazotoa mikopo kwa wanawake na kwa vijana zimekwisha ainishwa

- Maombi ya mkopo yanaendelea kuwasilishwa katika SACCOS husika

6.Bima ya Afya

Zoezi hili halijaanza
 Eneo la Soko la ndizi ndani ya soko kuu Mjini Bukoba.
Taswira Stendi kuu ya Mabasi Mjini Bukoba .
Next Post Previous Post
Bukobawadau