Bukobawadau

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAASWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WAWEKEZAJI NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza Vifungashio kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi, Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha na kulia ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akisaini kitabu cha wageni alipofika katika kiwanda cha kutengeneza Vifungashio kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru (Katikati), Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga(kushoto)  na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha wakielekea ndani ya kiwanda kuangalia mitambo na hatua iliyofikiwa kabla ya kuanza kazi ya kiwanda hicho.