Bukobawadau

WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI MULEBA

Na mwandishi wetu
Muleba
WATU wanne  wamefariki dunia  na majeruhi wengine 14 katika ajali  ya gari iliyotokea eneo la Nundu-Katoke wilayani  Muleba mkoani Kagera baada ya gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajiri T832 lililokuwa linaendeshwa na bwana Omar Twaha  (40) kupinduka na kupotea njia.
 
Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoani  Kagera Agustino Ollomi alisema kuwa tukio hilo lilitokea novemba 07 mwaka majira ya saa 1:10 jioni wakati watu hao walipokuwa wakitoka msibani  ndipo walipofika eneo la Nundu katoke kutokana na mwendo kasi lililokuwa nalo gari hilo lilipasuka tail la nyuma la kulia  na kuacha  kupinduka.
 
Ollomi aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na Evodius ambaye amekufa papo hapo aliyetambulika kwa jina moja ambaye mwili wake umehifadhiwa katika kituo cha afya Kaigara, Diana Pius aliyefia katika hospitali ya Rubya, Edmundi Fidelis na Renatus Vedasto miili yao imetunzwa katika hospitali ya Kagondo.
 
Alisema  majeruhi watatu hali zao ni mahututi ambao ni Thobias Titus (28) fundi wa vioo Rwamishenyi ,  Max   Hanta (45) na Rweyemamu Frediricki  wote wakazi wa Rwamishenyi  ambao wamelazwa  katika hospitali ya Kagondo na madakitari wanaendelea  kuwahudumia ili kuokoa maisha yao na majeruhi wengine kumi na mmoja wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Kagondo.
 
Kamanda Ollomi aliongeza kuwa , chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na mwendo kasi  wa huyo dreva na gari lilipata pancha taili ya nyuma mkono  wa kulia na baada ya tukio dreva ametoroka na novemba 08  mwaka huu alikamatwa   na atafikishwa mahakamani.
 
Hapo hapo,   Perepetua Julius  (32) amekutwa amekufa  katika tarafa ya Rulenge  wilayani Ngara baada ya kupigwa na kitu kizito kichani.
 
Aidha Kamanda huyo wa polisi mkoani Kagera Agustino Olomi alieza juu ya tukio hilo  na kusema kuwa, marehemu  amekutwa amekufa akiwa ametupwa kichakani umbali wa mita 100 kutoka anapoishi.
 
Aliongeza kuwa , mnamo novemba 04 mwaka huu majira ya saa nne usiku marehemu aliondoka nyumbani kwake hakuonekana tena hadi  alipokutwa amepoteza maisha novemba 07 mwaka huu na uchunguzi umebaini kuwa alipigwa kitu kizito kichwani.
 
Amesema mtu mmoja ambaye ni mume wa marehemu  aliyefahamika kwa jina la Julius Saimon Sengiyunva anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na tukio hilo baada ya kuwepo ugomvi wa muda mrefu baina ya marehemu na mume wake.
Next Post Previous Post
Bukobawadau