Bukobawadau

MAREJESHO YA MIKOPO YANAKWAMA KUTOKANA NA HALI YA UCHUMI NA ATHARI YA TETEMEKO

Na Mwandishi Wetu
Bukoba.
WANACHAMA wa ushirika wa Bukoba tuinuane women Saccos (BUTUWOSA) Ltd wamesema kutokea kwa majanga ya tetemeko la ardhi na njaa imewasabisha kushindwa kurejesha mikopo yao kama inavyotakiwa na kwa wakati.

Kaulii hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Saccos hiyo Marygleth Mgisha katika taarifa yake aliyoisoma mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano mkuu wa nne wa ushirika huo uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa santa theleza mjini Bukoba.

Hata hivyo "tunayo mafanikio mambali toka Saccos yetu ianzishwe 2001 ila zipo changamoto tunazo kabiliana nazo ikiwemo wanachama pamoja pamoja na vikundi kushindwa kurejesha vizuri kwasababu ya kipindi hiki kuwa kigumu hasa kuwa na janga la tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10/9/2016 na wengi wao kukosa makazi na sehemu ya kufanyia biashara pia mzunguko wa fedha kuwa mgumu" alisema Mgisha

Mgisha alisema kuwa vikundi kulalamika kutopewa fedha za kukopeshwa kwa wakati kwa sababu ya ucheleweshwaji wa fedha kutoka manispaa ya mwishowe inakuwa ni vurugu pamoja na kero za simu kwa meneja kuhusu fedha hizo.

Vikundi kutopewa semina au maelezo toka Manispaa wakidhani ni pesa za kutolewa tu bila kufuata masharti ya ushirika pia masharti yake kuwa magumu kwa sababu ya kuhitaji kuweka dhamana ya hati ya nyumba kinyume na taratibu zetu za Saccos pia na kuzungushwa sana wakati wa kutolewa cheki.

Mgeni lasimi wa mkutano huo ambae ni Meya wa manispaa ya Bukoba mkoani kagera Chifu Karumuna alisema kuwa wanachama wa ushilika wanatakiwa kushilikiana kikamilifu ili kuongeza wanachama vikundi na mwanachama mmoja mmoja ili kuuikuza Saccos.

Meua huyo alisema kuwa ushirika uliokuwa umefikia wanachama 291 na kubakiwa na wanachama 160 ikiwa vikundi vilikuwa 41 na kwa sasa vikundi vikundi 13 vimekufa na kubakia vikuni 28 tu.

"Ndugu wanaushilika wa (Butuwosa) mnatakiwa kujua kuwa mda wa siasa umekwisha hivyo kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa bidii pasipo kuutumia muda mwingi kupiga maneno na baada ya kufanya kazi za uzalishaji ili tuweze kukopoa na kulejesha biba kuburuzwa"alisema Chifu Karumuna

Karumna alisema kuwa pesa zinazotolewa na manispaa ya Bukoba sio zawadi zinapotolewa kwaajili ya kuwasaidia vijana na wanawake mwisho zinatakiwa kulejeshwa.

Aidha meneja wa Saccos hiyo Regina Allon alisema kuwa hadi sasa wamepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 28,118,346.50 kutoka katika manispaa ya Bukoba zikiwa ni fedha za kukopesha vikundi vya akina mama ikiwa ni fedha inayolejeshwa ndani ya mwa mmoja na una riba ya asilimia kumi ambayo inabaki kwenye ushilika huo.

"Akina mama niwe mkweli kila mwanachama ajitahidi kuweka hisa za kutosha hata zaidi ya 100 pamoja na akiba ili saccos yetu ikuwe vinginevyo haitakuwa itaenderea kuwa changa siku zote"alisema Allon.
Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau