Bukobawadau

TAARIFA KUTOKA KWA RPC KAGERA

Na  mwandishi wetu
Bukoba.

MTOTO  Junior Bosco mwenye umri wa  miezi mitano na wiki mbili  afariki dunia kwa ajari ya kuungua na moto ndani ya nyumba ya wageni iliyopo  mwalo wa igabilo kata ya Kaagya Halmashauri wilaya  Bukoba  mkoani kagera baada ya kuachwa na mama yake lilian Johnsen (21) mkazi wa Nyakibimbili na kwenda kuangalia televishen iliyokuwa mapokezi ya nyumba hiyo.


Hayo yalisemwa na kamanda wa polisi mkoani hapo Agostine Ollom alisema kuwa,tukio hilo lilitokea desemba 9 mwak huu majira ya 2:usiku ambapo mtoto huyo alikuwa amelala kwenye nyumba kilichokuwa kimejengwa kwa mabanzi na kuezekwa kwa bati.


Kamanda Ollomi alisema kuwa, nyumba hiyo yenye jina la Upendo  ambayo ni mali ya Damian Benedicto iliungua na kutekekeza mali zote zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo baada ya jitihada za kuzima moto huo kushindikana.


Pia alisema kuwa mtoto huyo alikuwa amelala chumba na 25 ambako mama yake alikifikia sehemu hiyo kwa ajiri ya shughuli zake katika mwalo huo.


Aidha alisema kuwa chanzo cha moto huo hakijajulikana mpaka sasa na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kujua tatizo hilo lilisababishwa na nini.
Mwisho.Next Post Previous Post
Bukobawadau