Bukobawadau

WANANCHI KAGERA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO TUNAPOELEKEA MWAKA 2017

Askofu Abedinego Keshomshara Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -KKKT

Na mwandishi wetu 
Bukoba

WANANCHI mkoani Kagera wametakiwa kudumisha upendo na amani na utulivu pamoja na mshikamano hasa tunapo elekea mwaka mpya wa 2017.

Kauli hiyo imesemwa  na Askofu Abedinego Keshomshara wa kanisa la kiinjiri la kiruthe Tanzania(KKKT) dayosisi ya kasikazini Magaribi wakati alipokutana na waandishi wa habari ofisini kweke mjini Bukoba zikiwa zimbakia siku tatu ya kusherehekea kuzaliwa kwa kristo.

Alisema kuwa katika kudumisha upendo ni pamoja na kubadilika na kutubu na kumugeukia mungu pamoja na kusameheana pale watu wanapo fanyiana mabaya katika maeneo yote kuanzia ngazi ya familia.
Keshomushahara alisema kuwa upendo huleta ukaribu  na kutokuwa na mipaka ya ukabira, kutokuwa na mipaka ya lika dini au masikini na tajiri' 

"wahaya wana methali inayosema kuwa watu hulingana na wote ni sawa mbele ya kifo na wote ni sawa  hata katika kabuli liwe limejengwa kwa heshima zote ndani ni uozo,Uozo wa tajili katika kabuli niuleule sawa na wa masikini katika kabuli kwanini tofauti ziwepo kabula ya kifo chetu zikisubili usawa baada ya kifo chetu maana yake nini maana yake tusiishi kwa kubaguana kwa jambo lolote kwa kuwa kifo kina tufanya tuwe sawa basi tuwe sawa hata kabla ya kifo" alisema Askofu huyo.

Askofu alisema kuzaliwa kwa yesu kristo kumaanishe kujali maendeleo ya afya maana yesu aliponya watu wengi tujali afya wanaomwa waende hospitali na tuepuke imani zinazo waambia watu kuwa waombe tu eti wasiende hospitali maana watu wengi wamepoteza  maisha  kwa imani hiyo maana kuna walipangiwa kupona kwa kuomba au hospitali na wakati mwingine vyote kwa pamoja.
"Yesu anasema ombeni pia anasema tafuteni huyo huyo anasema bisheni hivyo kuna muda wa kuomba na kuna muda wakutafuta huduma za kimaendeleo na tuepuke mafundisho ambayo yanaweza kutupotosha na kutuondoa katika kujali afya zetu.

Kuzaliwa kwa Yesu kumaanishe kujali elimu maana Yesu alikuwa mwalimu mzuri aliewataka watu wabadilishe tabia zao na kuweza kuza matunda mema yao binafisi na matunda mema ya familia na jamii kwa ujumla 

Kuzaliwa kwa yesu  kumaanishe kuwa wachapa kazi katika maeneo ya kazi maofini mashuleni,vyoni hospitalini, katika kilimo, ufugaji na biashara na hapo tutakuwa tumeunga mkoano kauli mbiu ya  hapa ni kazi tu na kwa njia hiyo tulenge kuzalisha zaidi na zaidi.

Krismasi hii itoe changamoto ya kufanya kazi kwa bidii zaidi ya hapo awali , kwani hali ya kitabia ya nchi zimekuwa nyingi ukame umetokea , tetemeko la ardhi limetokea na kusababisha madhara mengi ambayo yamesababisha watu kukosa makazi na nyumba nyingi zinanyufa.
mwisho. 
Next Post Previous Post
Bukobawadau