Bukobawadau

WANNE WAFARIKI DUNIA WAKATI WA SIKU KUU YA KRISMASI



WATU wa nne wamefariki Dunia katika matukio tofauti tofauti mkoani Kagera wakati wasikuku ya krisimasi
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi mkoani Kagera Augustine Ollomi wakati alipokuwa akitoa taarifa ya matukio kwa vyombo vya habari mjini Bukoba.
Hata hivyo kamanda huyo aliyataja majina ya marehemu hao kuwa ni Dodo Jastine (30) mkazi wa chanika kata kanoni wilayani Karagwe .
Marehemu huyo alikutwa amekufa katika shamba la miti Faustini Bwile akiwa amejeruhiwa sehemu za kichwa.
Wakati huo huo wilayani Biharamulo tarehe 25 mwaka huu Sudhana (42) mkazi wa Kanuguru tarafa ya Nyarumbugu aliuliwa na mumewe kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kuvuja damu nyingi na kuperekea kifo chake na mwanaume huyo kutokomea kusikojulikana.

Aidha mtu mwingine alikutwa amekufa na mwili wake ukiwa umetutwa katika barabara ya nyakanazi mkazi wa Ntumagu nyanza Rusahunga wilayani biharamulo majina yake Kigozi Saimoni (66)
Kamanda Ollomi aliongeza kuwa mtu mwingine Iziraeli Rugarabamu (52) mwalimu wa shule ya msingi Ombwea Kata kabilizi Halmashauli ya Bukoba alikutwa amejinyonga majira ya saa moja ambapo mkewe Prisika ndie alie mgundua akiwa amejinyonga na kamba ya katani sebuleni wakati alipokuwa akitoka kanisani.
'Mke wa marehemu alijinyonga alisema alikaata kwenda kanisani na kubakia nyumbani kwa madai kuwa alikuwa anaumwa vidonda vya tumbo na hata katika familia hakukuwa na ugomvi wa aina yoyote.
"Mpaka sasa vifo vyote vinne hatujua chanzo chake tunaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha matukio hayo"alisema Kamanda Ollomi
Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau