PAPA FRANCIS KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA KANISA LA KILUTHERI
Papa Francis |
Na Richard Mwaikenda
KIONGOZI Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 500 ya kuasisiwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.
Taarifa hiyo imetangazwa leo wakati wa Ibada ya Jumapili ya kuukaribisha mwaka mpya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule Ukonga, Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yatafanyika hivi karibuni eneo ambapo kanisa hilo liliasisiwa nchini Ujerumani ambapo kutakuwa na shamrashamra za kila aina zitakazoshuhudiwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kwa hapa nchini maadhimisho hayo yatafanyika katika Chuo cha Dini cha Makumira, mkoani Arusha, ambapo mnara wa kumbukumbu utajengwa. Kanisa hilo liliasisiwa mwaka 1557.