Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na
balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule
hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani
humo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati
Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe
kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo
mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa
uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya
Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi
huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
wa ukaguzi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
ukaguzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika
shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake
mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo
kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo
wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo
ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha
wageni pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa mkutano katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali
Mstaafu Salum Kijuu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera hawapo pichani mara baada ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera hawapo pichani mara baada ya kukagua na
kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa
mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakitoka kwenye ukaguzi wa
shule ya Sekondari Omumwani mkoani Kagera. PICHA NA IKULU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
MARA NYINGI NYAKATO HUWA HAITAJWI AU HAIKUATHIRIKA SANA? AU MIPANGO IKOJE?
Post a Comment